Habari za Punde

Fainali ya Kombe la Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Zanzibar Kati ya Chuo Kikuu cha Tunguu na Chuo cha Fedha Chwaka.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud, akiwasili katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kuhudhuria sherehe za fainali ya Michezo ya Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe.
Meneja wa Bank of Africa Tawi la Zanzibar Ndg.Juma Burhan akisoma risala wakati wa fainali za Michuano ya Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Zanzibar Bank of Africa, imedhamini michuano hiyo ya Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Zanzibar. 
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe Rashid Ali Juma akizungumza wakati wa fainali hizo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwahutumia wanamichezo wa Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Zanzibar wakati wa maadhimisho ya mashindano hayo wakati wa mchezo wa fainali kati ya Chuo cha Fedha Chwaka na Chuo Kikuu cha Tunguu Zanzibar mchezo uliofanuika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Chuo Kikuu Tunguu imeshinda kwa mabao 4--2. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Chuo Kikuu cha Tunguu Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa fainali na Timu ya Chuo cha Fedha Chwaka.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Kiongozi wa Kamati ya Michezo hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Chuo cha Fedha Chwaka Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa fainali na Timu ya Chuo cha Tunguu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.