Habari za Punde

PBZ Yatimiza Miaka 50 Kwa Shughuli Mbali mbali za Kusaidia Jamii Zanzibar.


Jengo la Msikiti lililojengwa kwa Nguvu za Wanafunzi, Walimu na Wazee wa Skuli ya Mwanakwerekwe C Unguja likiwa katika hali ya kuezekwa baada ya kupokea msaada kutoka PBZ wa Vifaa vya Uwezekaji wa Msikiti huo na bado kunahitajia Msaada kwa ajili ya umaliziaji wa Msikiti huo ili kuweza kutowa huduma kwa Waumini wa Dini ya Kiislam kuweza kuutumia kwa Ibada,  Uongozi wa Skuli hiyo Unaomba misaada kwa Wanainchi ili kukamilisha ujenzi huo. Kwa Mawasiliano ya kuchangia Msikiti huo unaweza kuwasiliana na Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Mwanakwerekwe C Ndg. Hassan Abass kwa No 0773164227.   
Meneja Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg. Mohammed Nuhu akizungumza na waandishi wa habari weakati wa kutembelea Ujenzi wa Msikiti huo wa Skuli ya Mwanakwerekwe C Unguja baada ya kukabidhi Msaada wao wa Vifaa vya Ujenzi kwa ajili ya kuezeka Msikiti huo. ili kuweza kutowa huduma ya Ibada kwa Wanafunzi na Jamii ya Jirani na eneo la Skuli hiyo ikizingatiwa Skuli hiyo ni moja ya Matumizi makubwa wakati wa shughuli mbalimbali za Kijamii hivi karibuni skuli hiyo ilikuwa imewekwa Kambi ya Wananchi waliopata Maafa ya kujaa kwa maji majumba yao. 
Meneja Masoko wa PBZ Ndg Mohammed Nuhu akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Mwanakwerekwe C Unguja Mwali Hassan Abass akitowa shukrani kwa msaada wa Vifaa vya kuezekea vilivyotolewa na PBZ, ili kufanikisha kuweza kuezeka jengo hilo la Mskiti na kuomba michango kwa Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar kufanikisha ujenzi huo kwa michango yao.
Mwalimu wa Skuli ya Mwanakwerekwe C Unguja Mwalimu Abdalaa Mohammed Shirazi akishukuru na kuwataka Wananchi kuchangia ujenzi huo wa msikiti kuweza kutowa huduma kwa Jamii ya Ibada msikitini hapo. na kupunguza utoro wa Wanafunzi wa Skuli hiyo wanayoitowa wakati wa kwenda kusali itakuwa shida hiyo imewaondokea na wanafunzi watuwa katika eneo hilo na kupata ibada wakati ikifika.
Mwalimu wa Skuli ya Mwanakwerekwe C Unguja akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhia vifaa vya ujenzi na PBZ kwa ajili ya kupaua paa la Msikiti huo na kuwataka Wananchi kuchangia Msikiti huo wa Skuli na Jamii ya jirani na Skuli hiyo na kusisitiza kuwaomba Wananchi waliopata barua zao za kuoba msaada kuwasaidi katika sehemu iliobakia katika msikiti huo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.