Habari za Punde

Jumuiya ya Kanga Maternity Trust yafanya semina na kutoa taarifa za kitafiti kuhusu wajawazito na ugonjwa wa Saratani

 Daktari bingwa. Tarek Meguid wa wodi ya Wazazi Mnazimmoja Hospitali akitoa tarifa ya pili ya watafiti wazalendo kuhusu wajawazito na watoto katika Semina ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust iliyofanyika Tembo Hotel Mjini Zanzibar.
 Dkt. wa Maradhi ya Saratani Mnazimmoja Hospital Salama Uledi Mwita akitoa taarifa ya hali ya ugonjwa wa Saratani ulivyo sasa Zanzibar katika Semina ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust.
 Dkt. Sanaa S. Said, Physician (Internal medicine) Mnazimmoja Hospital akiuliza swaali kwa watafiti wazalendo (hawapo pichani) katika Semina iliyofanyika Tembo Hotel Mjini Zanzibar.
 Dkt. Msafiri Marijani akitoa ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa kuhusu ugonjwa wa Saratani (kushoto) Dkt. Salama Uledi Mwita ambae amewasilisha tafiti ya ugonjwa wa Saratani ulivyo Zanzibar.
 Dkt. Mdhamin wa Kijiji cha Watoto (S.O.S) Zanzibar Abdulla Mohammed Hassan akimkabidhi Certificate Dkt. Natasha Hussein kwa niaba ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Madaktari bingwa wa Hospitali ya Mnazimmoja, (kulia) Dkt. Tarek Meguid na (kushoto) Dkt. Msafiri Marijani wakiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kanga Maternity Trust (KMT) wa katikati Dk. Mohammed Hafidh wakifuatilia uwasilishwaji wa Tafiti za ndani kwa madaktari wazalendo.
 Baadhi ya walikwa katika Semina ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust. Picha na Makame Mshenga /Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.