Habari za Punde

Kiwanda cha Chuma cha MMI Steel Mokocheni Jijini Dar es Salaam Chatozwa Faini ya Shilingi Milioni 10

Na Evelyn Mkokoi. Dar es Salaam.
Kiwanda nda cha kutengeneza vyuma cha MMI Steel kilichopo katika eneo la viwanda mikocheni jijini Dar es Salaam, kimetozwa faini ya shilingi milioni kumi na kutakiwa kulipa faini hiyo baada ya siku saba kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira na kanuni zake ya mwaka 2004, kwa kutiririsha maji machafu katika maeneo ya mtaa wa TPDC kwa warioba jijini dar es salaa. Maji ambayo ni hatari kwa mazingira na viumbe hai.

Adhabu hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa 

Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea eneo la  mtaa wa viwanda mikocheni kufuatia uchafuzi wa mazingira unaotokanao na utitiririshaji wa majitaka katika maeneo hayo.

Wakati huohuo, Shirika la maji safi na majita taka Jijini Dar es 

Salaam na Pwani  ( Dawasco) limepewa siku kumi na saba 

kumaliza tatizo la utiririshaji wa maji taka katika mtaa wa TPDC 

mikocheni kwa Warioba jijini Dar es Salaam.


Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri Mpina Baada ya 

kufanya usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi wa tatu na kutoa 

siku saba kwa DAWASCO na NEMC kusimamia suala zima la 

usafi wa mazingira na agizo lake kuupuzwa.

Awali, Mhe. Mpina alisema kuwa uchafuzi wa mazingira hauwezi 

kuendelea kuvumiliwa na lazima hatua za kisheria zichukuliwe, na 

kuwaasa watendaji wa taasisi za serikali kuyapa kipaumbele 

maagizo yanayotolewa na viongozi wa ngazi za juu za serikali 

kinyume na hapo ni kutokutii mamlaka. “tasisi za serikali lazima 

zifanye kazi kwa kushirikiana kutokana na kwamba kumekuwa na 

kutupiana mpira kati ya NEMC, dawasco na Manispaa ya 

kinondoni katika suala zima la utatuzi wa uchafuzi wa mazingira 

katika mtaa wa TPDC.” Alisema.

Naibu waziri Mpina aliongeza kuwa  ifikapo tarehe 30/7/2016  

asikutane tena na tatizo la uchafu na harufu mbaya katika mtaa wa 

TPDC kwani hali hiyo ni hatari sana kwa afya ya wakazi wa 
maeneo hayo na mazingira.

Kwa upande wake DAWASCO ikiwakilishwa na Injinia Erick 

Jackson alisema kuwa Tangu muheshimiwa Naibu Waziri Mpina 

atoe agizo la uondoshwaji wa majitaka na uboreshwaji wa 

miundombinu katika mtaa huo, wamekuwa wakifanya kazi na 

bado inaendelea na kazi hiyo  pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali za kifedha na ufundi.


Hata hivyo uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya kinondoni 

umelishitaki shirika la maji safi na maji taka jijini dar es salaam na 

Pwani DAWASCO ,kiwanda cha MMI steel na Tembo Tiles kwa 

uchafusi wa mazingira kwa kutirirsha maji taka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.