Habari za Punde

Msimu mpya wa uvunaji karafuu, uanikaji sahihi na usiokuwa sahihi wa zao la karafuu

 UANIKAJI bora wa karafuu kwa kutumia majamvi, huipatia hadhi karafuu ya Zanzibar katika soko la dunia, pichani karafuu zikiwa zimeanikwa katika majamvi katika eneo la Mtambile Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba, wakati msimu mpya wa uchumaji wa zao hilo ukiwa umeanza, jambo ambalo husaidia karafuu hiyo ya mkulima kuingia katika gredi ya kwanza.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
LICHA ya Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) kutoa taaluma kwa wananchi juu ya uwanikaji bora wa zao la karafuu kwa kutumia majamvi, baadhi ya wakulima wa zao hilo wamekuwa wakienda kinyume na taaluma hiyo, picha karafuu mbichi zikiwa zimeanikwa katika maturubali katika shehia ya Changaweni Wilaya ya Mkoani, huku msimu mpya wa uvunaji wa zao hilo ukiwa umeanza.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.