Kamisheni ya Wakf na Mali ya Amana Zanzibar inawatangazia nafasi za masomo ya Uimamu na Ualimu wa madrasa chini Algeria kwa muda wa miaka 3 kwa ngazi ya diploma na digrii .
Sifa za muombaji
1. Awe amehitimu kidato cha nne.
2. Awe anajua kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiarabu kwa ngazi diploma na kwa ngazi digirii awe amehetimu kwa ngazi ya shahada ya mwanzo na sifa nyengine zilotajwa hapo juu
3. Barua ya maombi iambatanishwe na vivuli vya vyeti vifuatavyo:-
1. Cheti cha kuzaliwa,
2.Kitambulisho cha Uzanzibari na
3. Cheti cha kumalizia masomo
4. Maombi yote yaandikwe kwa mkono na yaelekezwe kwa Katibu Mtendaji Kamisheni ya Wakf na Mali ya Amana Zanzibar. Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi hayo ni tarehe 20/07/2016.
Ahsanteni.
No comments:
Post a Comment