Habari za Punde

SMZ kukiimarisha kituo cha elimu mbadala

Na Maryam Kidiko –Maelezo 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuchukuwa juhudi ya kusaidia Kituo cha Elimu Mbadala na Watu Wazima ili kuweza kuimarika zaidi na  kupata kuwasaidia kusoma  vijana mbali mbali waliokosa kuendelea na masomo yao.

Ameyasema hayo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  Riziki Pembe Juma katika maazimisho ya kutimiza miaka kumi tokea kuanzishwa kwa Kituo cha Elimu Mbadala na Watu Wazima huko Raha leo Mjini Zanzibar.

Amesema kufanya hivyo ni kuwasaidia vijana mbali mbali kama vile Walemavu , waliokatisha masomo yao,Waliopata ujauzito {mimba za utotoni } pamoja na Watu Wazima waliokosa Elimu toka mwanzo. 

Aidha amesema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar inatarajia kujenga Vituo mbali mbali  kama hivyo kwa Unguja na Pemba ili kuweza vijana kujiajiri wenyewe na kupunguza idadi kubwa ya vijana wasio na ajira.

“ Vijana wengi hawana ajira hivyo tunaendelea kuchukuwa juhudi za kuwasaidia kwa njia ya kuanzisha vituo mbali mbali vinavyofundisha ujasiria mali ili kuhakikisha vijana wanaweza kujiletea maendeleo wenyewe bila kutegemea Serikali” Alisema Waziri huyo.


Hata hivyo amesema Wizara pia itaendelea kuwasaidia walimu kwenda kupata mafunzo ya uwalimu katika vyuo mbali mbali ili kuweza kupata ujuzi zaidi wa kusomesha .

Waziri wa Elimu amewataka wanafunzi mbali na changamoto zinazowakabili katika masomo yao wasikate tamaa na wachukuwe juhudi kubwa ya kuendelea na masomo yao.

Sambamba na hayo amewaomba pia watu wazima waliokuwa hawajasoma kwenda kujiunga na kituo hicho ili kupata elimu kwa kuwa    elimu ndio ufunguo wa maisha  na wala  haina mwisho .
.
Nae mMurugenzi wa Kituo cha Elimu Mbadala na Watu Wazima Mashavu Ahmada Fakihi amesema kituo hicho kimesaidia watu wengi zikiwemo taasisi na vijana kupata kuepuka kujiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya na mambo yasiyofaa katika jamii.

Vile vile amefahamisha kuwa kituo hicho kimesaidia sana kuelimisha jamii juu ya suala zima la kuweza kujiajiri wenyewe kwa kutumi a elimu inayotolewa hapo pamoja na kuepuka wimbi kubwa la uzururaji kwa vijana.

“ Vijana wengi waliosoma katika kituo chetu wameweza kupata  ajira Serikalini, katika makampuni mbali mbali na wengine kujiajiri mwenyewe” Alisema mkurugenzi Mashavu.
Pia ameeleza kuwa wanafunzi wengi wameweza kuwabadilisha tabia zao zilizokuwa sio nzuri sambamba na kuwawezesha wale waliokuwa hawajui kusoma na kuandika.
Akieleza changamoto zinazokikabili Kituo chake ni pamoja na ukosefu wa vitendeya kazi , usafiri, uhaba wa sehemu ya kufundishia na kufanyia mazowezi.

Maazimisho hayo yameambatana na maonyesho mbali mbali yaliyoandaliwa na wanafunzi wa kituo hicho ikiwa ni  miongoni mwa maonyesho hayo  kama vile ushoni,mapishi pamoja na ufundi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.