Habari za Punde

Kuwasili kwa Mwili wa Rais Staaf wa Zanzibar Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi Zanzibar leo kwa Mazishi Nyumbani Kwake Migombani.

Wakati wa uhai wake Rais Mstaaf wa Zanzibar Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi. 
Ndege iliochukuwa Mwili wa Marehemu Rais Mstaaf wa Zanzibar Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi ikiwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar ikitokea Jijini Dar es Salaam, alipofariki na kusafirisha kuja Zanzibar kwa mazishi nyumbani kwake Migombani Zanzibar Maziko yamefanyika leo mchana. saa saba. 
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakiwa wabebeba jeneza lililokuwa na Mwili wa Rais Mstaaf wa Zanzibar Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kwa mazishi leo mchana. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na Viongozi na Wananchi wakiupokea mwili wa Rais Mstaaf wa Zanzibar Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.
Viongozi wa Serikali na Wananchi wa Zanzibar wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kuupokea Mwili wa Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi ulipowasili leo ukitokea Jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Wananchi wagine wakiitikia dua ya kumuombea Marehemu Mzee Aboud Jumbe Rais Mstaaf wa Zanzibar, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume. leo mchana kwa mazishi nyumbani kwake migombani Zanzibar.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh, Saleh Omar Kabi akisoma dua baada ya kuwasili mwili wa marehemu Rais Mstaaf wa Zanzibar Aboud Jumbe Mwinyi.
Mwili wa Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ukiwasili katika nyumba yake migombani Zanzibar. kwa ajili ya mazishi hayo.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.