Habari za Punde

Kwa Mwenendo huu wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora Sijui!

Na Mwandishi Wetu.

Wakati ligi kuu ya soka Zanzibar hatua ya nane ilipotaka kuanza, mashabiki wengi walionekana kuzipa nafasi timu mbili kongwe za soka kutoka kisiwani Pemba nafasi ya kupambana na timu za vikosi vya ulinzi vya SMZ.


Imani hiyo ilikuja kutokana na kwamba timu za Jamhuri na Chipukizi ziliwahi kushiriki ligi kuu ya soka visiwani hapa miaka miwili iliyopita tofauti na wenzao wa Mwenge na African Kivumbi.


SUPER EIGHT PREMIER LEAGUE ZANZIBAR 2015-2016
POS
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
ZIMAMOTO
7
5
2
-
16
3
13
17
2
KVZ
7
5
1
1
13
5
8
16
3
JKU
7
4
2
1
11
5
6
14
4
JAMHURI
7
2
3
2
8
7
1
9
5
MAFUNZO
7
2
2
3
11
9
2
8
6
CHIPUKIZI
7
2
1
4
9
12
-3
7
7
MWENGE
7
1
3
3
6
11
-5
6
8
AFR/KIVUMBI
7
-
-
7
4
26
-22
-

Jumla ya mabao 78 yamefungwa kupitia michezo 28 ambayo imeshachezwa


Wafungaji:
Ibrahim Hamad           6  Zimamoto
Emmanuel Martin       5  JKU
Hakim Khamis            5  Zimamoto
Suleiman Hassan         4 KVZ

Rashid Abdalla            4 Mafunzo
Mbali na hayo pia timu hizo mbili zilishawahi kuiwakilisha Zanzibar kwenye mashindano ya kimataifa.

Aidha Jamhuri na Chipukizi ni timu ambazo zimeonekana kuwa na viongozi wanaoweza kuzisimamia vyema ili kuleta ushindani uwanjani wakiungwa mkono sana na mashabiki wao.

Lakini chakushangaza timu hizo zimeonekana kuwa kinyume na matarajio yaliyowekwa na mashabiki wao.

Mzunguko wa kwanza wa ligi kuu hatua hiyo ya nane bora umekamilika kwa kila timu kucheza michezo saba.

Kimsimamo wa ligi bado nafasi ipo kwa timu hizo kufuta machozi ya wafuasi wao sambamba na kutafuta angalau nafasi moja ya kuiwakilisha Zanzibar kwenye mashindano ya kimataifa barani Afrika.

Ikiwa hili litashindikana, basi mzigo huo utabaki kwa vilabu vinavyomilikiwa na vikosi vya ulinzi na usalama yaani Zimamoto, KVZ, JKU na Mafunzo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.