Habari za Punde

Serikali Itahakikisha Mabaraza ya Vijana Yanafanya Kazi na Kujikwamua Kiuchumi

Na Maryam Kidiko - Maelezo.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itashirikiana na mabaraza ya vijana ili kuhakikisha kwamba mabaraza hayo yanafanya kazi na kujiletea maendeleo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Hayo ameyasema Waziri wa kazi uwezeshaji wazee vijana wanawake na watoto Mhe. Maudline Cyrus Castico wakati akizinduwa Baraza la Vijana la Wilaya ya Mjini huko katika Ukumbi wa Rahaleo Mjini Zanzibar.

Amesema mabaraza hayo yameanzishwa kwa lengo la kuwaweka  vijana pamoja ili kujadili mambo mbali mbali na kuweza kutatua  changamoto zinazowakabili pamoja na kuweza kujiajiri wenyewe.

“Mabaraza haya hajali rangi, kabila, Dini wala chama chochote kila mtu anahaki ya kujiunga bila ya ubaguzi wowote kutokea,” amesema Waziri Castico.

Waziri huyo  amefahamisha kuwa kuna baadhi ya ya watu hawana uwelewa wa  kuwepo kwa mabara hayo hivyo  amelitaka Baraza la Vijana Wilaya ya Mjini kuwa  mfano wa kuweza kutoa elimu kwa vijana wenzao.

Aidha ameeleza kuwa kuna baadhi ya  vijana wamejiingiza katika vitendo viovu hivyo ipo haja kubwa ya kupewa elimu itakayoweza kuwashawishi kuachana na vitendo hivyo kwani vijana ndio nguvu ya Taifa.

Waziri Castico amesema Wizara yake ipo tayari  kuwasaidia vijana kwa kuwapatia mikopo ili waweze kuanzisha miradi itakayoweza kuwaingizia kipato kitakaweza kujikwamua kimaisha.

Sambamba na hayo Waziri huyo amefahamisha kuwa vijana  wana umuhimu mkubwa wa kuendeleza na kukuza mila na tamaduni za kizanzibari kwa kutumia vipaji mbali mbali walinavyo kwani vipaji hivyo ndio chanzo cha kujiletea maendeleo.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Maua Makame Rajab amewataka Vijana kushirikana kwa pamoja na kutumia vyema fursa hiyo  waliyoipata na kujitolea kufanya kazi kwa hali na mali katika mabaraza hayo kwa lengo la kuleta maendeleo nchini.

                                             
           IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.