Habari za Punde

Asilimia kubwa ya mapato yaishia mifukoni Bandari ya WeteNa Salmin Juma - Pemba

Kaimu mkuu wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali amezitaka taasisi husika katika bandari ya wete kushirikiana kwa pamoja katika utendaji wao wa kazi ili kusaidia kupatikana kwa mapato ya serekali.

Akizungumza na watendaji wa bandari hiyo chini ya kamati ya ulinzi na usalama Ndugu Abeid Juma Ali ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Micheweni , ameelezea kutoridhishwa na ukusanyaji wa mapato ambapo amedai kwamba asilimia kubwa yanaishia mifukoni mwa wachache .

Amesema amebaini bandarini hapo kutokuwepo na ushirikiano kati ya taasisi zinazofanya kazi hapo ambapo na kushindwa kutekeleza wajbu na majukumu yao kwa pamoja .

Aidha amewataka watu wa usalama bandarini kuhakikisha wanaimarisha ulinzi bandarini hapo ili kupunguza uingiaji na utokaji kiholela katika bandarini hiyo.

Hata hivyo serekali ya wilaya imepiga marufuku kwa vyombo vya mashua vinavyofanya safari kutoka pemba kwenda tanga kutobeba abiria hadi hapo taarifa nyengine zitakapotolewa .

Kwa upande wake Afisa forodha pemba Suleiman Abdalla Said amesema kua ipo haja kwa watendaji wa bandari hiyo kufanyiwa mabadiliko ya ndani ili kupunguza changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza.

Nae Kaim mkurugenzi wa bandari Pemba Abdalla Kassim Shimeli ameeleza kuwa wamejiandaa na utaoji wa sare kwa watendaji wote ambao wanafanya kazi katika eneo hilo ili kudhibiti uhalifu bandarini hapo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.