Habari za Punde

Karata ya Kwanza kwa Zanzibar Queen jana Imeanza kwa Kufungwa na Timu ya Taifa ya Burundi Mabao 10-1

Mashindano ya Cecafa Women Championships yanatarajia 
kufungua dimba hapo kesho kwenye dimba la njeru, jijini 
Jinja nchini Uganda.
Kikosi cha Zanzibar Queens wakipasha asubuhi ya leo kabla ya mchezo wa kesho dhidi ya Burundi

Pazia la mashindano ya Cecafa Women Championships linatarajiwa kufunguliwa mchana wa leo kwenye dimba la njeru jijini Jinja, nchini Uganda.

Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo leo hii kutakua na Michezo miwili ambapo saa nane mchana Zanzibar Queen wataanza karata yao kwa kuchuana na Burundi.

Mara baada ya pambano hilo ufunguzi rasmi la ufunguzi litapigwa kati ya wenyeji wa mashindano Uganda dhidi ya Kenya.

Kocha msaidizi wa Zanzibar Queen Mustafa Hassan alisema kikosi chake kina ari kubwa kuelekea pambano hilo.

"Vijana wapo sawa, mbinu za wapinzani tumezipata na nimezifanyia Nazi naamini kama watafuata maelekezo ushindi utapatikana".

Mashindano hayo yanayoshirikisha timu za taifa za mpira wa miguu za wanawake yanafanyika kwa mara ya kwanza chini ya mwavuli wa Baraza hilo la mpira wa miguu kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.