Habari za Punde

Kikosi cha Timu ya Zanzibar Queens Kutangazwa leo Jumapili.

Kikosi cha wachezaji 18 kitakachounda timu ya taifa ya  Zanzibar kwa upande wa soka la Wanawake kinatarajiwa kutangazwa rasmi jumapili ya kesho kutwa majira ya saa  nne asubuhi uwanja wa Amaan.
Kocha msaidizi wa kikosi cha 

Zanzibar  Queens Mustafa Hassan 

maarufu KOCHA Muu alisema 

mchakato wa kuwapunguza 

wachezaji hao kutoka 26 hadi 18 

umeanza.

"Vijana wanaendelea na mazoezi 

wakati wa asubuhi uwanja wa 

Amaan na Jumapili tutataja majina 

18 ya wachezaji ambao watasafiri" 

alisema Kocha Mkuu.

Kikosi hicho kitaiwakilisha Zanzibar 

kwenye mashindano ya Cecafa Women championship nchini 

Uganda kuanzia September 11-20 mwaka huu wa 2016.

Zanzibar imepangwa kundi A ikiwa na timu za taifa za 

Burundi, Kenya na wenyeji Uganda.

Kundi B linaundwa na Tanzania bara, Rwanda pamoja na 

Ethiopia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.