Habari za Punde

Mafunzo ya ukusanyaji kodi kwa maofisa wa taasisi za Serikali Kisiwani Pemba

 Ofisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Saleh Haji Pandu, akitowa mada juu ya kodi ya zuwio ambayo inapaswa kutolewa na watowa huduma.
 Ofisa kutoka TRA-Pemba, Ariff Moh'd Said akiwa pamoja na ofisa wa ZRB-Zanzibar, Safia Is-haka Mzee, wakifuatilia kwa makini mafunzo ya ukusanyaji kodi kwa maofisa wa taasisi za Serikali Kisiwani Pemba, ambayo yalikuwa yanatolewa na Saleh Haji Pandu.


Ofisa kutoka ZRB - Zanzibar, Makame Khamis Moh'd ,akiwasilisha mada juu ya marekebisho ya Sheria za Kodi kwa maafisa wa Taasisi mbali mbali za Serikali Pemba.
 Washiriki wa Semina ya ukusanyaji Kodi kutoka taasisi mbali mbali za Serikali Kisiwani Pemba, wakiwa makini kusikiliza mada zinazotolewa kutoka kwa maafisa wa TRA na ZRB , huko katika ukumbi wa hoteli ya Archipelago, Pemba.
 Mhasibu wa JKU Pemba, akiuliza maswali kutoka kwa maafisa wa kodi kutoka TRA na ZRB, huko Kisiwani Pemba.
 Katibu wa Baraza la Mji Chake Chake Pemba, akiuliza maswali kutoka kwa maofisa wa kodi wa TRA na ZRB, katika Semina iliyoandaliwa kwa taasisi mbali mbali za Serikali Pemba.
 Ofisa kutoka TRA Pemba, Arif Moh'd Said, akiwasilisha mada juu ya usajili na Uhakiki  wa namba ya utambulisho wa biashara TIN namba.

Ofisa kutoka ZRB Pemba, Safia Is-haka Mzee, akifunguwa mafunzo ya ukusanyaji kodi kwa maofisa wa taasisi mbali mbali za Serikali juu kutowa mashirikiano  kwa taasisi zakodi ili kufanikisha ukusanyaji wakodi kwa maslahi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Picha na Bakar Mussa -Zanzibarleo Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.