NA TAKDIR ALI. MAELEZO . 23-09-2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuifanyia ukaguzi mitaala ya Skuli za binafsi ili kwenda sambamba na mitaala ya Skuli za Serikali.
Hayo ameyasema leo huko Uwanja wa Amani mjini Zanzibar wakati akihutubia wananchi katika maadhimisho ya miaka 52 ya elimu bila malipo.
Amesema mitala ya skuli za binafsi haiendi sambamba na ile ya serikali kitu ambacho hakipaswi ,hivyo amesema ikohaja ya Wizara ya elimu namafunzo ya amali Zanzibar kushirikiana katika kuangalia mitaala miataala hiyo ya ufundishaji ili iende sambamba na skuli za serikali.
Aidha amesema mashirikiano ya pamoja yapande hizo mbili yatapelekea wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao ya majaribio na ile ya mwisho wa mwaka.
Dkt. Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga vyema katika kuhakikisha kwamba inakabiliana na changamoto mbalmbali zinazoikabili sekta ya elimu hapa Zanzibar ili kuhakikisha inafikia dhana ya Raisi wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume alioitangaza Elimu bila malipo mwaka 1964.
Akiwazungumzia Wazazi juu ya suala zima laelimu kumpatia mtotoDkt. Ali Mohamed Shein amesema suala la elimu kwa mtoto hali mlazimu mwalimu pekeyake bali ni jambo la wote ambalo linahitaji ushirikiano kati ya mwalimu wazazi na wanafunzi.
Amesema wasiachiwe walimu pekeyao kufundisha na kuwaongoza bali wae na ushirikiano wa pamoja.
Pamoja na hayo Dkt.Ali Mohamed Shein alisema kabla ya Mapinduzi ya Mwaka1964 ilimu Zanzibar ilikuwa ikitolewa kwa misingi ya ubaguzi kituambacho kiliwafanya wonyonge kuikosa hakihiyo ya elimu kitu ambacho kwa sasa Zanzibar imepiga hatua kubwa mbele kwani upatikanaji wa elimu ni wa kila mmoja ambae kafikia umri wa kwenda skuli.
Ameseama haki hiyo sasa imefikiwa kukua nakwasaa kua na vyuo vikuu vitatu kwa ujumla wake mbapo kwa kiasi ya miaka 20 iliopita Zanzibar haikuwa na hata chuo kikuu kimoja na kupelekea wanaotaka kusoma kuenda nje ya Tanzania.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment