Habari za Punde

Israel yataka ushirikiano na Afrika katika usalama na teknolojia

 Waziri Mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyau alipokutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya   viongozi wa  nchi za Afrika wanaohudhuria Mkutano wa  71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Katika  mkutano huo   Waziri Mkuu alieleza baadhi ya maeneo ambayo  angependa nchi yake ishirikiane na  nchi za Afrika
 Waziri  wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika Mshariki akiwa na Mwakilishi wa Kudumu wa  Tanzania katika  Umoja  wa Mataifa, wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Israel  Benjamin Netanyau alipozungumza na  baadhi ya   Viongozi wa Afrika.
Waziri Mkuu Netanyau  akibadilishana mawili  matatu na  Waziri Mahiga mara baada ya kumalizika kwa mkutano


Na Mwandishi Maalum, New York

Katika kile kinachoonekana  kwa Israel kuendelea na mchakato wa kutaka kuwa karibu na Nchi za Afrika,  jana ( Alhamis) Waziri Mkuu wa  nchi hiyo,  Bw. Benjamin Netanyau alikutana  na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi  wa nchi  za Afrika  wanaohudhuria  Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Vipaumbele ambavyo Waziri  Mkuu amevieleza mbele  ya viongozi hao  pamoja na  mambo mengine  katika maeneo ya  za usalama  na teknolojia.

Tanzania ikiwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga  ni kati ya nchi za Afrika zilizoalikwa kuhudhuria  na kushiriki mkutano huo. Dkt Mahiga  anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa  71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Akichangia vipaumbele hivyo  vya Israel kwa Afrika,  Waziri Mahiga amesema   usalama na  teknolojia ni  mambo muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote ile na hususani zinazoendelea.

“Israel  imetambua kuwa  usalama na  teknolojia ni    maeneo muhimu ambayo nchi zetu zinaweza kushirikiana. Na sisi Tanzania tungependa kuyatambua   maeneo  hayo kwa sababu  ni kweli  ulinzi na teknolojia ni nyenzo muhimu kwa maendeleo”. Akasema Balozi Mahinga

Akaeleza kwamba kinachotakiwa  kuanzia  baada ya  mkutano huo  uainishaji wa  namna gani  ya kuanza majadiliano  iwe  kati ya Israel na nchi moja moja ( bilateral ) au kwa  katika mfumo wa   majadiliano ya  kikanda.

Vyovyote vile itakavyokuwa  Waziri  Mahiga amesisitiza kwamba,   majadiliano hayo lazima yawe jumuishi, yasiyobagua na yenye manufaa kwa pande zote mbili. Kauli  iliyopigiwa makofi na   washiriki  wengine ikiwa ni ishara ya kuiunga mkono.

Netanyau alikuta  na viongozi hao  muda mfupi mara baada ya kulihutubia  Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa, ambapo   baadhi ya  mambo aliyoyagusia kwenye  hotuba yake   na  kuyazungumzia kwa kirefu ni  uhasama  unaoendelea baina ya Israel  na  Palestina.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.