Habari za Punde

Serikali yaombwa kufufua kitengo cha Idara ya ushirika

Na Salmin Juma Pemba

Serikali imeombwa kukifufua kitengo cha idara ya ushirika wizara maalum au kama kipo basi kiweze kusimama na kufanya wajibu wake kwa kuona umuhimu wa uwepo wa vikundi vya ushirika katika jamii na hasa kwa kuwa vyama vya ushirika vya mkoa vipo.

Hayo yamesemwa hapo jana na mwenyekiti mpya wa chama kikuu cha ushirika mkoa Kusini Pemba (MKOCHA) Bw: Nassor Suleiman Nassor mara baada ya uchaguzi mkuu wa chama hicho kupitia mkuu huko katika ukumbi wa skuli ya maandalizi Chanjaani njia ya airport.

Amesema ni vyema serikali ikarejesha kitengo hicho kwa kuwa ndio  mlezi mkuu wa vyama vya ushirika ili kufanya wajibu wake na malengo yaliyokusudiwa kupitia vyama hivyo kuweza kufikiwa.

Amesema malengo makuu ya vyama vya ushirika ni kuona wananchi kupitia vyama hivyo  anajikwamua kimaisha na kuondokana na umasikini na kupiga hatua za kimaendeleo ila bado amesema serikali inaonekana haijatilia nguvu uwepo wa vyama hivyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi nje ya kikao hicho Mgeni rasmi katika ghafla hiyo bw: Kassim Ali, Omar afisa mipango ofisi ya mkuu wa wilaya Chake, amesema amelipokea shauri hilo na amesema atalifikisha katika ngazi husika na kukaa na viongozi wengine kulijadili  suala hilo ili kuona siku moja linasimama na kufanikiwa.

Kupitia mkutano huo uliweza kufanyika uchaguzi mkuu kwa viongozi mbali mbali wa chama hicho kikuu cha ushirika mkoa MKOCHA na kufanikiwa kupatikana kwa mwenyekiti mpya na wajumbe 7 wa bodi ya   mkoa na wajumbe 3 watakaowakilisha mkutano mkuu taifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.