Habari za Punde

Waziri Asiye Kuwa na Wizara Maalum Zanzibar Mhe Ali Juma Khatib Akabidhi Msaada wa Vyakula Kituo cha Sober House Mpendae Zanzibar.

 
Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe Ali Juma Khatib akabidhi msaada wa Vyakula kwa Vijana wa Nyumba ya Sober House Mpendae Zanzibar, kwa ajili ya Vijana hao kupata huduma nzuri wakati wakiwa katika nyumba hiyo kupata ushauri nasaha wa kuacha matumizi ya Dawa za Kulevya Zanzibar akipokea Msaada huo Kiongozi wa Nyumba hiyo Ndg Mohammed Mahfoudh Chuluu, wakishuhudia Vijana wa Sober hiyo ilioko Mpendae Unguja.


 Kiongozi wa Nyumba ya Sober House Zanzibar Ndg Mohammed Mahfoudh Chuluu, akitowa shukarani kwa Mhe Ali Juma Khatib kwa msaada wake huo wa vyakula kwa Vijana wa Nyumba hii kwa Vijana wanaopata tiba ya kuachana na matumizi ya Dawa za Kulevya Zanzibar na kuwataka Wananchi na Wafanya biashara kutowa michango yao kwa Vijana hao wanaoachana na matumizi ya dawa na kurudi katika jamii kuimarisha nguvu kazi.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.