Habari za PundeJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA JIJI ARUSHA
Barua zote zitumwe kwa:
            Mkurugenzi wa Jiji,
            20 Barabara ya Boma,
Simu:

Nukushi:
+255 27 2548072/2503494 (Director)
+255 27 2544330 (General)
+255 27 2545768
             S. L. P.  3013,
             23101 ARUSHA,
Barua Pepe:  cd@arushacc.go.tz
Tovuti:  www.arushacc.go.tz
Unapojibu tafadhali taja:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ndugu 

Athuman J. Kihamia anapenda kukanusha na kutoa 

ufafanuzi juu ya taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya 

kijamii kuhusu matumizi ya mafuta lita 1900. Halmashauri 

ya Jiji la Arusha ina jumla ya Idara 13 na Vitengo 5. Idara ni 

Utawala, ujenzi, Fedha, Elimu Msingi, Elimu Sekondari, 

Maendeleo ya Jamii, Afya, Usafishaji na Mazingira, 

Mipango miji, Mipango   Takwimu na Ufuatiliaji na Maji. 

Vitengo ni Ugavi, Ukaguzi wa Ndani, Sheria na Uchaguzi. 

Katika Idara zote kuna jumla ya magari 48 mitambo 5 na 

wastani wa matumizi ya mafuta kwa Idara zote ni lita 18,900 

kwa mwezi na Idara zenye matumizi makubwa ni ujenzi na 

usafishaji na mazingira hii inatokana na Idara hizi kutumia 

idadi kubwa ya malori na mitambo katika kutekeleza 

shughuli zake.  Mafuta yanaweza kununuliwa kwenye vituo 

binafsi endapo itatokea dharura na GPSA inakosa mafuta na 

manunuzi yatafanywa kwa kuzingatia bei isiyozidi viwango 

vya GPSA.

Baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema wanasambaza  

taarifa hizo katika mitandao ya kijamii kutokana na juhudi 

mbalimbali ambazo Mkurugenzi amekuwa akizifanya za 

kutatua kero mbalimbali kwa kubana matumizi yasiyokuwa 

ya lazima zikiwemo posho mbalimbali za watumishi na 

Waheshimiwa Madiwani. Fedha nyingi huelekezwa katika 

huduma mbalimbali za jamii kama vile afya na elimu.

Hata  hivyo kumekuwepo baadhi ya watu wasiokuwa 

waaminifu ambao wamejipanga kuchafua kila jambo jema 

linalofanywa na Mkurugenzi wa Jiji nia yao kuu ikiwa ni 

kumtoa kwenye lengo kuu la kuwahudumia wananchi bila 

ubaguzi wa aina yoyote, kusimamia miradi ya maendeleo 

na matumizi ya fedha zinazotokana na kodi za wananchi na ruzuku toka Serikali Kuu zilizokuwa zikitumika kinyume na utaratibu.

Aidha Mkurugenzi  Kihamia amekuwa akipokea jumbe za 

vitisho na matusi kutoka kwa baadhi ya Madiwani lengo 

likiwa ni kudhoofisha juhudi anazozifanya za kuliweka  Jiji 

katika mstari.

Tangu Mkurugenzi Kihamia alipoteuliwa  amekuwa 

akisisitiza kufuatwa kwa kanuni, sheria, taratibu na 

miongozo na kuwachukulia hatua wale wote waliokwenda 

kinyume na utaratibu ikiwepo kurejeshwa posho 

zinazolipwa kinyume na taratibu kwa Madiwani wa 

Halmashauri ya Jiji la Arusha na kufuta posho zisizokuwa 

za lazima zilizokuwa zikilipwa kwa Maafisa mbalimbali wa Jiji. Pia anatoa rai kwa watumishi wa Jiji wenye tabia yakutoa nyaraka za Serikali kinyume na sheria na kusambazwa katika mitandao ya jamii waache tabia hiyo kwani kosa la jinai na atakayegundulika  atawajibika kwa mujibu wa sheria zilizopo. Ndugu Kihamia ameahidi kuwa kumchafua katika mitandao ya kijamii hakutapunguza dhamira yake ya kuwahudumia wananchi kwa weledi na uadilifu  kwa kutenda  haki bila kumwonea mtu yeyote.

Tangu alipofika Jiji la Arusha mwezi Julai 2016 Mkurugenzi 

hajawahi kuidhinisha mafuta, wala posho kwa ofisi ya 

Mkuu wa Wilaya, wala kwa Mkuu wa Mkoa ambazo hazikuhusiani na shughuli za Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Hivyo wananchi  wanaombwa kupuuza taarifa hizo kwani 

hazina ukweli wowote na zina lengo la kumchafua  

Mkurugenzi huyu.

Frank R. Sanga
Afisa Tawala, Halmashauri ya  Jiji
Arusha.

05 Oktoba 2016

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.