Habari za Punde

Watumishi 3 Wasimamishwa kazi, Arusha



Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo, amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za uchaguzi wa mwaka 2015. 

Na Mwandishi wetu,
Watumishi hao ni pamoja na Bi. Hadija Mkumbwa ambae alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa mwaka 2015 na kumfuta  cheo hicho,bwana Evansi Mwalukasa alikuwa mwekahazina wa halmashauri na  bwana Sembeli Sinayo yeye alikuwa mwanasheria wa halmashauri.
Maamuzi hayo yamefikia baada yakubainika kuna upotevu  wa fedha za uchagu takribani Milioni 188 ambazo matumizi yake hayakuwekwa  wazi na pia Milioni 20 zilitumika kwa manunuzi ambayo hayakufuata taratibu za manunuzi ya serikali.
“Kuanzi sasa nawasimamisha  kazi hawa watumishi watatu kwasababu wameisababishia serikali hasara ya takribani Milioni 128 ambazo zilikuwa fedha za uchaguzi”.
Aidha Muheshimiwa Gambo alisema maamuzi hayo yametokana na taarifa aliyokabidhiwa na kamati aliyoiunda yakuchunguza mapato na matumizi ya fedha za halmashauri hiyo na kubaini upotevu huo wa fedha nyingi ambazo zingeweza kusaidia shughuli mbalimbali za uchaguzi katika Wilaya hiyo.
Ambapo fedha nyingine zimetumika kwenye manunuzi ambayo hayakufuata taratibu na sheria za manunuzi ya serikali ,hivyo ni kinyume kabisa na taratibu za serikali katika maswala ya manunuzi.
Akisisitiza kwa watumishi wa serikali kufuata taratibu, sheria na kanuni mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ili kuepuka migongano na uvunjifu wa sheria mahala pa kazi nakupelekea kupoteza kazi  zao.


Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Ngorongoro wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani),alipokuwa akizungumza nao baada yakufanya ziara katika ofisi za halmashauri hiyo, Wilayani Ngorongoro.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.