Na.Kauthar Abdalla
Waziri ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar imesema itahakikisha ushirikiano zaidi
unatolewa baina ya walimu na wadau katika mradi wa ikolijia maskulini (Eco
schools) ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Waziri
wa elimu na mafunzo ya amali Zanzibar, Riziki Pembe Juma aliyasema hayo wakati
wa ufunguzi wa mkutano wa tatu wa kimataifa wa nchi za visiwa duniani zilizomo
kwenye mradi wa "Eco schools".
Aidha
alisema ushirikiano huo atahakikisha unatolewa katika sekta za umma na binafsi ili kila moja iwe na mchango katika
mradi huo.
Alisema
Wizara pia itashirikiana na wadau hao ili kuhakikisha program inapata wataalam
na vifaa vinavyostahili kwani jukumu la kulinda mazingira ni la wote.
Alifahamisha
kuwa programu ya Eco ina lengo la kuwawezesha wanafunzi, vijana na watoto kuwa
na wajibu wa kuyaenzi Mazingira.
Nae
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Vijana Elimu na Mazingira,
(ZAYEDESA) mama Shadya Karume alisema ipo haja kwa walimu wa maskuli mbali
mbali kuubeba mradi huo hasa skuli za Serikali kwa kuwaelimisha wanafunzi
wayatunze mazingira ili itunzwe hali ya
hewa na ardhi ya nchi hii.
Alisema endapo
mazingira yatatunzwa, nchi itakuwa na uwezo wa kuzalisha chakula hata katika
maeneo ya skuli kwa kupanda vyakula kwa kuwa mazingira ndio sehemu ya maisha.
Hata
hivyo Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya kusimamia mazingira, (ZEMA) Sheha Mjaja
Juma alisema suala la uhifadhi wa mazingira linafanana na nchi mbali mbali
duniani hasa suala la udhibiti wa taka.
Sambamba
na hayo alisema changamoto kubwa katika mazingira ni uchukuaji mali asili
zisizorejesheka kutokana na uelewa mdogo wa jamii.
Mradi
wa Ikolojia katika skuli za ukanda wa bahari ya Hindi maarufu kama "Eco
Schools" unaratibiwa na Kamisheni ya Bahari ya Hindi (IOC) chini ya
ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya (EU), uliletwa nchini na Wizara ya Ardhi Maji
Nishari na Mazingira nakuratibiwa na Jumuiya ya Mandeleo ya Vijana, Elimu na Mazingira,
Zanzibar (ZAYEDESA) chini ya utekelezaji wa kamati ya kitaifa ya
ZNSC iliyozishirikisha taasisi mbalimbali za umma na binafsi kwa ushirikiano na
Wiraza ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar.
No comments:
Post a Comment