Habari za Punde

Jamii Imetakiwa Kuwajengea Ustawi Mzuri wa Maisha Watoto.

Na.Salmin.J.Salmin.Pemba.
Jamii imetakiwa kuacha tabia zinazoweza kuwanyima watoto haki zao za msingi na badala yake wawajengee  ustawi mzuri wa maisha  ya baadae.

Afisa mdhamini wizara ya fedha na uchumi Pemba Ibrahim Saleh Juma ameyasema hayo huko ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Pemba alipokuwa akizindua kitabu cha muongozo wa mabaraza ya watoto chenye lengo la kuimarisha haki na wajibu katika kutoa maamuzi juu ya mambo yanayohusu.

Amesema kuna baadhi ya wazazi na walezi huwavunjia haki watoto kwa kuwaozesha na kuwakosesha elimu ya msingi jambo ambalo huleta migogoro miongoni mwa jamii.

Katika risala yao watoto hao wameiomba Serikali na viongozi wengine kuyapa kipaumbele masuala ya watoto kwa kuimarishwa ulinzi utakaosaidia kuondoa vitendo vya unyanyasaji kwa watoto hao .

Wamesema  mabaraza yamekuwa yakikabiliwa na changamoto nyingi hivyo ni budi kwa serikali kuwategea bajeti itakayoweza kuboresha hali ya mabaraza hayo ili lengo la uzinduzi wa kitabu hicho liweze kufanikiwa.

Akielezea lengo la kitabu hicho mwekiti wa badi ya ushauri ya  baraza la watoto Zanzibar Mundhir Hamad Said amesema kupitia muongozo huo watoto watapata fursa ya kuachwa huru kutoka katika mazingira  hatarishi na vitendo vya udhalilishaji kutoka kwa jamii .

Uzinduzi huo wa kitabu cha muongozo wa mabaraza ya vijana Zanzibar umefadhiliwa na shirika na huwahifadhi watoto ulimwenguni la Save the children kikiwa na kauli mbiu ya kulindwa , kushirikishwa ,kupata hifadhi ,chakula, afya bora na kuelimishwa .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.