Habari za Punde

MAKUMBUSHO YA WATU WA ZAMANI KUUMBI, JAMBIANI YAFUNGULIWANaibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Chum Kombo Khamis akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Makumbusho ya watu wa zamani yaliopo Kuumbi Jambiani, Mkoa Kusini Unguja. 
Mtafiti wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Professa Felix Chami wa kwanza (kulia) akitoa maelezo juu ya utafiti uliofanywa na kupelekea kuanzishwa kwa makumbusho ya Kuumbi Jambiani.
 Mkuu wa Divisheni ya Mambo ya Kale Zanzibar Abdallah Khamis Ali akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utalii Utamaduni na Michezo Chum Kombo Khamis wa kwanza (kushoto) wakati wa ufunguzi wa makumbusho ya Kuumbi.
Naibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Chum Kombo Khamis akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa Idara ya Makumbusho wakati wa ufunguzi wa Makumbusho ya Kuumbi, Jambiani Mkoa Kusini Unguja.
Baadhi ya wananchi na wafanyakazi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale walioshiriki ufunguzi wa Makumbusho ya Watu wa zamani Kuumbi wakifuatilia  sherehe hizo.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.