Habari za Punde

Rais Joseph Kabila wa Jamuhuri ya Kidomokrasia ya Congo Amaliza Ziara yake Nchini Tanzania na Kurejea Nchini Kwake Baada ya Ziara ya Siku Tatu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni  wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini na kurejea DRC.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kabla ya kuondoka. Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakati akimsindikiza katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kabla ya kuondoka. Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakati nyimbo za Taifa za mataifa yote mawili zikipigwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakiangalia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikitoa burudani uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakiangalia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikitoa burudani uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akipunga mkono wakati akipanda ndege kurejea nchini kwake mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu hapa nchini 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakipunga mkono kuagana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila (hayupo pichani) katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu akikagua mashine ya ukaguzi wa mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal One kuangalia ufanisi wa mashine hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu akiangalia ufanisi wa mashine za kukagulia mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal One na kukuta zinafanya kazi vizuri. Aliyekaa ni Mwendeshaji wa Mashine hizo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege TAA-Grace Jonathan.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.