Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID), imekutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini pamoja na wadau katika kuboresha miundombinu, semina iliyofanyika mapema jana Oktoba 19 katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Semina hiyo iliyofunguliwa na mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo, Bw. Juston Lyamuya aliipongeza UTT-PID kwa namna ilivyoweza kubobresha miundombinu pamoja na shughuli za kimaendeleo hususani katika upatikanaji wa viwanja na hati kwa wananchi kwenye miradi yake mbalimbali hapa nchini.
“Sote kwa pamoja tunaipongeza UTT-PID, kwa namna inavyoendesha shughuli zake hasa katika sehemu mbalimbali za Halmashauri, Miji na Manispaa kwani zimeboresha miundombinu na hta wananchi kufaidika na miradi hii ambayo ipo kwa uwazi sambamba na kuendeshwa kisasa” amesema Mgeni rasmi huyo.
Katika semina hiyo, mada mbalimbali zimewasilishwa na wadau ikiwemo miradi ya upamaji ardhi, miundombinu, ujenzi na fursa zilizopo katika maeneo ya Majiji, Miji na Halmashauri hapa nchini.
Aidha, Manispaa ya Lindi ilipongezwa kwa namna ya kipekee kufikia malengo katika miradi yake na UTT-PID Kwani ubia wao huo umekuwa wa mafanikio makubwa.
Naye Mkurugezi wa Manispaa ya Lindi Jomary Satura wakati wa kuwasilisha mada katika semina hiyo juu ya fursa za uwekezaji zinazopatikana katika manispaa hiyo, amewaomba wananchi na wadau kujitokeza kwa wingi Manispaa ya Lindi ilikunufaika zaidi na fursa zilizopo.
























No comments:
Post a Comment