Habari za Punde

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwame Azungumza na Wanawake wa UWT Wilaya ya Kaskazini A Unguja

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Viongozi wa UWT wakati akiwasili katika viwanja vya jengo la Mkorea Kibokwa Unguja kuzungumza na Viongozi na Wawanchi wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja.

Msoma risala ya Wananchi na Viongozi wa UWT Wilaya ya Kaskazini A Unguja Bifaida Salmin akisoma risala hiyo kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja katika ukumbi wa jengo la Mkorea Kibokwa Unguja. 
Kaimu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Kondo akizungumza na kuutambulisha Ujumbe wa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.wakati wa mkutano wake na Viongozi hao wa UWT Wilaya ya Kaskazini A Unguja kutowa shukrani zake kwao. 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Muasisi wa Umoja wa Wanawake Zanzibar Mama Fatma Karume akitowa nasaha zake kwa Vionongozi wa UWT Wilaya ya Kaskazini A Unguja, wakati wa mkutano huo, katika ukumbi wa jengo la mkorea kibokwa Unguja.
Baadhi ya Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM Zanzibar wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mlezi wa Umoja huo Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Viongozi wa UWT Wilaya ya Kaskazini A Unguja katika ukumbi wa mkorea kibokwa Unguja. 
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, na Mwenyekiti wa Umoja wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM Zanzibar. akitowa nasaha zake kwa viongozi hao wa UWT Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati wa mkutano wa Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Ujumbe wa Umoja wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM Zanzibar. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia na kutowa nasaha zake kwa Viongozi wa UWT Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati wa mkutano wake huo uliofanyika katika ukumbi wa mkorea kibokwa Unguja.
Wananchi wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akitowa shukrani kwa Viongozi hao wa UWT Wilaya ya Kaskazini A Unguja. kwa kuwachagua wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu uliopita Zanzibar.
Viongozi wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakimshangilia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mawanamwema Shein, wakati akizungumza na viongozi hao na kutowa nasaha zake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mkorea kibokwa Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.