Habari za Punde

Nafasi za kazi ya Ualimu

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA UALIMU SKULI YA JKU MTONI

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi za Walimu wa Sanaa na Sayansi kwa ajili ya kufundisha Skuli ya JKU Mtoni kama ifuatavyo:-

1. Afisa Elimu Sanaa Daraja la Pili (Mwalimu wa Sanaa) katika ngazi ya ZPSH – 07 kwa masomo yafuatayo:-

NAM. MASOMO            IDADI YA NAFASI
1           DINI                          2
2           ARABIC                   2
3           ENGLISH                 1
4           HISTORY                 2
5           CIVIC                       1
6           KISWAHILI              2
7          GEOGRAPHY           1
JUMLA 11

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Sanaa ya Ualimu kati ya moja ya masomo yaliyotajwa hapo juukatika Chuo kinachotambuliwa na Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar.

Majukumu ya Kazi:

• Kufundisha katika Skuli ya Sekondari hadi katika Kidato cha Sita.
• Kutunga, kusimamia na kusahihisha mitihani kwa lengo la kutathmini maendeleo ya wanafunzi.
• Kuandaa na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya wanafunzi.
• Kushiriki katika shughuli za utayarishaji wa mitaala, Silabi za Masomo kwa kila baada ya muda
inapobidi.
• Kutayarisha andalio la masomo


2. Afisa Elimu Sayansi Daraja la Pili (Mwalimu wa Sayansi) katika ngazi ya ZPSH – 09 kwa masomo
yafuatayo:-

NAM.                  MASOMO                           IDADI YA NAFASI
1                          BIOLOGY                                 1
2                          CHEMISTRY                             2
3                          MATHEMATICS                       2
4                          PHYSICS                                   2
5                          BOOKEEPING                          2
6                          COMMERCE                             2
7                          COMPUTER                              1

JUMLA 12

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya ya Ualimu wa sayansi kati ya moja ya masomo yaliyotajwa hapo juu katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Majukumu ya Kazi:
• Kufundisha katika Skuli ya Sekondari hadi katika Kidato cha Sita.
• Kutunnga, kusimamia na kusahihisha mitihani kwa lengo la kutathmini maendeleo ya wanafunzi.
• Kuandaa na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya wanafunzi.
• Kushiriki katika shughuli za utayarishaji wa mitaala, Silabi za Masomo kwa kila baada ya muda
inapobidi.
• Kutayarisha andalio la masomo


3. Afisa Elimu Sayansi Msaidizi Daraja la Tatu (Mwalimu wa Sayansi) katika ngazi ya ZPSF – 05 “Nafasi moja”

Sifa za Muombaji:

• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya stashahada katika fani ya ‘IT’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Majukumu ya Kazi:
• Kufundisha Elimu ya Sekondari.
• Kutathmini maendeleo ya wanafunzi
• Kutunga, kusimamia na kusahihisha mitihani ya wanafunzi.
• Kutahini mitaala ya masomo anayofundisha.
• Kuandaa na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya wanafunzi.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-


KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.
• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini
iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba
wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-

a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya
Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe
18 Novemba, 2016 wakati wa saa za kazi.
• Muombaji anatakiwa aiainishe nafasi ya kazi anayoiomba kati ya zilizotajwa hapo juu vinginevyo
maombi yake hayatazingatiwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.