Habari za Punde

Salamu za Rambirambi za CCM Kufuatia Kifo cha Balozi Mstaaf Mzee Waziri Juma.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndg. Henry Shekifu kufuatia kifo cha Balozi mstaafu Mhe Waziri Juma, kilichotokea juzi tarehe 22 Novemba, 2016 jijini Dar es salaam.

Mhe Waziri Juma ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kwa muda mrefu, Katibu wa CCM ngazi ya Mkoa, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT), pia amekuwa msimamizi wa ujenzi wa reli ya TAZARA, 

Mkuu wa Mkoa, na Balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali.
Mhe. Waziri, atakumbukwa na wanachama wa CCM kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi na uimarishaji wa Chama chetu, na kwamba mchango wake katika kupigania na kuleta maendeleo hapa nchini utaendelea kuenziwa na kuthaminiwa na Watanzania.

Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu na kwake yeye ndio marejeo yetu. 
Imetolewa na:- 
                   
Christopher Ole Sendeka (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
24.11.2016

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.