Habari za Punde

Taasisi ya Doris Mollel na Vodacom Foundation Yatembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Mwakilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Tanzania Bi Doris Mollel akizungumza wakati wa kujitambulisha kwa Uongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmmoja Zanzibar, walipofika kutowa misaada kwa Wazazi waliojifungua Watoto Njiti katika hospitali hiyo wakishirikiana na Vodacom Foundation Bi Doris Mollel ni mmoja wapo wa watoto Njiti. Ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Watoto Njiti Duniani.  

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Vodacom Bi Jackline Materu akizungumza wakati wa mkutano huo na Maofisa wa Hospitali ya Mnazi Mmoja walipofika kukabidhi Misaada ikiwa ni kuadhimishi Siku ya Watoto Njiti Duniani.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar Dk Ali Salum Ali akizungumza na Ujumbe wa Vodacom Foundatio na Taasisi ya Doris Mollel uliotembelea Hospitali hiyo kwa kutowa misaada kwa Wazazi waliojifungua Watoto Njiti, ambao hawakutimia miezi Tisa.  


Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania wakimsikiliza Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja wakati wa hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.