Habari za Punde

Walimu watakiwa kuwa makini vitendo vya Liwati kwa wanafunzi

Na Salmin Juma - Pemba

Kutokana na hofu iliyotanda kwa baadhi ya wanajamii kisiwani Pemba ya uwepo wa vitendo vya liwati kwa watoto wadogo  hatimae walimu kisiwani visiwani humo wametakiwa kutofumbia macho vitendo hivyo na badala yake kuripoti sehemu husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria kwani taarifa zinaonesha kua vitendo hivyo vinaonekana kushamiri siku hadi siku mashuleni. 

Wito huyo umetolewa na afisa kitengo cha elimu mjumuisho na stadi za maisha Pemba, Khamis Haji Hamadi wakati akitowa mafunzo ya siku moja kwa walimu na wanafunzi juu ya athari za ndoa za utoto katika ukumbi wa shule ya Madungu sekondari Chake chake Pemba. 

Amesema wameanda mafunzo hayo maalum baada yatafiti zilizofanywa na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar na kugunduwa kuwa baado vitendo vya liwati na ndowa za utotoni vinazidi kushamiri nchini. 

Akitowa mafunzo juu ya athari ya mimba za utotoni afisa kitengo cha cha elimu mjumuisho na stadi za maisha Zanzibar amewataka wanafunzi kuwacha kutumia utandawazi vibaya kwa mambo yasiokua na  tija kwao na badala yake kutumia kwaajili ya masomo na si vyenginevyo. 

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki ktika mafunzo hayo, mwanafunzi Zainabu Habibu Ali kutoka shule ya Shamiani Sekondari ameiomba Wizara ya Elimu isisitie hapo na badala yake iwe na mwendelezo wa kutoa elimu siku hadi siku akisema kufanya hivyo kwa namna moja ama nyengineyo kutasaidia vikubwa kupunguza vitendo hivyo vichafu kwa watoto na wanafunzi.

Amesema ndoa za utotoni, mimba kwa wanafunzi ni kudumaza maendeleo ya taifa ukizingatia kua watoto ndio viongozi wa taifa la baadae.

Jumla ya wanafunzi 50 kutoka shule mbali mbali kisiwani Pemba wamepatiwa mafunzo hayo ikiwa lengo pia ni kuleta uwelewa na mwamko kwa wanafunzi hayo hatimae kutojiingiza katika vitendo hivyo vichafu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.