Habari za Punde

Mtoto Ummu Salama Salim anahitaji msaada wako
Kuna mtoto wa miaka 7,  anaitwa Ummu Salama Salim anaishi Mchangani Zanzibar.

Mtoto huyu kazaliwa hana sehemu ya kutolea haja kubwa. Hospitali ya Mnazi Mmoja pamoja na Muhimbili wameshindwa kumtibu lakini upo  uwezo wa kufanyiwa matibatu In chini ndia.

Mama wa mtoto huyu tayari amelifikisha suala hili Misikitini na michango inaendelea lakini kusema la ukweli japo kuwa watu wanajitahidi lakini bado michango hairidhishi

Kwahivyo tunawaomba watu wote walio ndani na nje ya Zanzibar watakaoguswa nahli ya mtoto huyu basi tumsaidie.

Wewe binafsi jifikirie Tumbo likikuuma tu hali yako inavyokua, Jee huyu mtoto mdogo inakuwaje? Mfikirie pia na mama wa mtoto huyu ulezi aliokuwa nao.

Nimefanikiwa kuwaona mama wa mtoto huyu, Ummu Salama na kunieleza hali halisi

 Gharama za matibatu ni Milioni 15 za kitanzania ni sawa na £6000 za Uingereza au dola 7500 za kimarekani.

Kwa wale walioko UK unaweza kutuma mchango wako kupitia

Saba Traders Sort 090128  Account 78395061 (Santander)

Au wasiliana na Balozi mob 07846255735

Tafadhali unapochangia kwa kutumia akaunti weka ref Abuu Zam.

Vilevile nijuulishe kwa whatsapp +447947468729.

Kwa wale waliopo USA, Europe au Gulf unaweza kutuma kwa kupitia Western Union Anapokea Abuu Zam Tafadhali nijuulishe kwa  whatsapp +447947468729.

Kwa waliopo Tanzania nipigie simu kwa whatsapp au simu Zantel +255777917870.

Au unaweza kuwasiliana na mama wa mtoto na kumtumia moja kwa moja wasiliana nae kwa +255777257269.

Shime ndugu zangu tujitahidi kumsaidia mtoto huyu kwani Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi Wasallam anasema Mwenye kumpunguzia Muislamu mwenzake mtihani katika mitihani ya kidunia, Allaah atampunguzia mitihani yake katika mitihani ya kidunia na akhera.


Siku ya mwisho kupokea michango ni Ijumaa tarehe 23/12/2016 Bi ithni Llaah

Wabillaahi Tawfiyq


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.