Habari za Punde

Waziri wa Habari, Utamaduni na michezo ateua wajumbe wa Bodi ya Shirika la Utangazaji ZBC

Waziri wa Habari Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC)

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Wizara hiyo Ameir Abdallah Ameir imesema walioteuliwa ni pamoja na Hassan Ali Hassan na Kombo Shaame Kai.

Wengine ni Aziza Saleh Mohammed, Ramadhan Omar Mohamed na Nassor Rajab Dachi.

Taarifa hiyo imefahamisha kuwa uteuzi wa Wajumbe hao umeanza Disemba 23, 2016.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.