Habari za Punde

Yanga Afrika Yaendelea Ubabe Katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cu Zanzibar kwa Kuendeleza Kipigo kwa Timu ya Zimamoto Baada ya Kutoka na Ushindi wa Mabao 2--0.

Waamuzi wa mchezo wa Yanga na Zimamoto wakiingia Uwanja na Timu hizo tayari kwa kuaza Michuano ya Kombe la Mapinduzi Mchezo uliofanyika jioni hii. Na Timu ya Yanga kutoka uwanja kwa ushindi wa mabao mawili dhidi ya timu ya Zimamoto.  
Wachezaji wa Timu ya Yanga wakiwa uwanjani wakisubiri kusalimiana na Mgeni rasmin wa mchezo huo.  
Wachezaji wa Timu ya Zimamoto wakiwa uwanjani wakisubiri kusalimiana na Mgeni rasmin wa mchezo huo. 
Mgeni rasmin wa mchezo huo Omar Said akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Yanga Afrika kabla ya kuaza kwa mchezo huo. jioni hii.
Mgeni rasmin akisaliomiana na wachezaji wa Timu ya Zimamoto kabla ya mchezo wao wa pili Kombe la Mapinduzi Cup. 
Wachezaji wa Timu ya Yanga Afrika wakisalimiana na Wachezaji wa Timu Zimamoto kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa Kundi A.  
Kikosi cha Timu ya Yanga Afrika kinachoshiriki Kombe la Mapinduzi Cup Zanzibar katika mchezo wake wa leo kwa kutoka na ushindi wa mabao 2--0 dhidi ya Timu ya Zimamoto.
Kikosi cha Timu ya Zimamoto kinashiriki Kombe la Mapinduzi Cup Zanzibar kilichokubali kwa mara ya pili kupokea kipigo kutoka kwa Timu ya Yanga Afrika.
Muamuzi wa Mchezo kati ya Yanga na Zimamoto Waziri akirusha shilingi kuchagua upande wa kuaza kwea Timu hizo.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga Saimon Msuva akimiliki mpira huku beki wa Timu ya Zimamoto Hassan Haji akijiandaa kumzuiya. Timu ya Yanga imetoka kwa ushindi wa mabao 2--0. 
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga Juma Mahadi akimpita Beki wa Timu ya Zimamoto Suleiman Said
Mchezaji wa Timu ya Yanga Juma Mahadhi akimpita Beki wa Timu ya Zimamoto Suleiman Said. wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi Cup Zanzibar mchezo uliofanyika Uwanja wa Aman Zanzibar.
Mchezaji wa Zimamoto Haji Nahoda akimiliki mpira huku mshambuliaji wa Timu ya Yanga Saimon Msuva akijiandaa kumzuiya katika mchezo huo.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga Saimon Msuva akiwapita mabeki wa Timu ya Zimamoto wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi Cup Zanzibar mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Yanga imeshinda 2--0. 
Wachezaji wa Timu ya Yanga wakimpongea mchezaji wao Saimon Msuva baada ya kuipatia timu yake bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo mnamo dakika ya 11 ya mchezo huo. baada ya kumpiga kazu kipa wa Timu ya Zimamoto Mwinyi Hassan.
Benchi la ufundi la Timu ya Zimamoto likiongozwa na kocha wake Seif Bausi wakifuatilia mchezo huo wao wa Poli wa Kombe la Mapinduzi Cup Zanzibar. mchezo wake wa kwanza wamefungwa na Timu ya Azam.
Mchezaji wa Timu ya Yanga akiweka majaro golini kwa timu ya Zimamoto wakati wa mchezo huo wa Kombe la Mapinduzi Cup.  

Mchezaji wa Timu ya Yanga Mwinyi Haji akipiga mpira huku beki wa Timu ya Zimamoto Shafii Hassan akijaribu kumzuiya. 
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga Saimon Msuva akishangilia bao lake la pili na la ushindi alilolifunga katika dakika ya 21 ya mchezi kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Mfungaji wa Bao la Pili la Yanga Saimon Msuva akipongezwa na mchezaji mwezake Juma Mahadhi, baada ya kuifungia timu yake bao la pili katika dakika ya 21 ya mchezo kipindi cha kwanza cha mchezo huo. 
Wapenzi wa mchezo wa Soka Zanzibar wakifuatilia mchezo wa kati ya Yanga na Zimamamo unaofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kipa wa Timu ya Zimamoto Mwinyi Hassan akidaka mpira huo huku mshambuliaji wa Timu ya Yanga Juma Mahadha akijaribu kuupiga mpira huo. huku mbeki wa Timu ya Zimamoto Suleiman Said akiwa tayari kutowa msaada kwa kipa wake.
Mshambuliaji wa Timu ya Zimamoto Ibrahim Hamad akiwapika wachezaji wa Timu ya Yanga kushoto Saimon Msuva na kulia Beki Mwinyi Haji.
Mshambuliaji wa Timu ya Zimamoto Ibrahim Hamad Hilika akimpita mchezaji wa Timu ya Yanga Saimon Msuva huku beki wa Timu ya Yanga Mwinyi Haji akijiandaa kumzuiya mchezaji huyo.
Mshambuliaji wa Timu ya Zimamoto Ibrahim Hamad Hilika akiwapita wachezaji wa Timu ya Yanga Saimon Msuva na Mwinyi Haji.

Benchi la ufundi la Timu ya Yanga wakifuatilia mchezo wao wa pili wa Kombe la Mapinduzi Cup.
Mshambuliaji wa Timu ya Zimamoto Ibrahim Hamad Hilika akimpita beki wa Timu ya Yanga Mwinyi Haji. 
Mchezaji wa Yanga Kiungo mkabaji  Haruna Niyozima akimpita mchezaji wa Timu ya Zimamoto Yussuf Ramadhani. 

Kizazaa golini kwa timu ya Yanga wakati wa mchezo wao na timu ya Zimamoto. 
Golikipa wa Timu ya Yanga Deogratias Muvishi Dida akiwa hewani akidaka mpira huo huku mabeki wake wakiwa makini kutowa msaada huku mshambuliaji wa timu ya Zimamoto Ibrahim Hamad Hilika akiwa tayari kuleta madhara.
Kocha wa Timu ya Zimamoto Seif Bausi akizungumza na waandishi wa habari akizungumzia mchezo wa timu yake kupoteza tena na kueleza bado wachezaji wake hawana uzoefu wa michezo mikubwa bado wanayo tamaa ya kusonga mbele katika michuano hiyo. 
Kocha wa Timu ya Yanga akizungumza na waandishi wa habari za michezo wanaoripoti michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Mgeni rasmin wa mchezo huo Omar Said akimkabidhi zawadi mchezaji Bora wa Mpambano huo wa Kombe la Mapinduzi Saimon Msuva. Kampuni ya Bahressa hutowa zawadi kwa Mchezaji Bora hukabidhiwa katuni nne za kinywaji cha Malti

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.