Habari za Punde

Waziri Haji Omar Kheir azindua jengo jipya la kituo cha Polisi Makangale kisiwani Pemba

 JENGO jipya la kituo cha Polisi Makangale Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, lililofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalumu za SMZ Mhe:Haji Omar Kheir, katika shemra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi, Kituo ambacho kimegharimu zaidi ya Milioni 53 hadi kukamilika kwake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 VIONGOZI mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za SMZ Mhe:Haji Omar Kheri, Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiimba wimbo wa taifa wa Zanzibar, mara baada ya kukifungua kituo cha Polisi Makangale ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 ASKARI wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakiwa wamesimama kwa ukakamavu wakiimba wimbo wa Taifa wa Zanzibar, mara baada ya kuzinduliwa kituo cha Polisi Makangale, ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya mapinduzi matukufu ya zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WANAFUNZI wa Skuli ya Makangale Salama Nassor na Sharifa Juma, awakisoma Utenzi katika shamra shamra za Uzinduzi wa Kituo cha Polisi Makangale, katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ, Mhe;Haji Omar Kheir, akizungumz ana wananchi wa Makangale mara baada ya kukifungua kituo cha Polisi Makangale katika shamra shamr za Miaka 53 ya Mapinduzi ya zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WANAFUNZI mbali mbali wa skuli ya sekondari na masingi makangale, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na idara Maalumu za SMZ, Mhe:Haji Omar Kheir, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa makangale katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za SMZ, Mhe:Haji Omar Kheir, akikunjuwa kitambaa kuashiria uzinduzi wa kituo cha Polisi Makangale, ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za SMZ, Mhe:Haji Omar Kheir, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo cha Polisi Makangale, ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Kituo cha Polisi Makanagle Ali Bakari Hamad kushoto, akimpatia maelezo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Mhe:Haji Omar Kheir, mara baada ya kukizindua Rasmi kituo cha Polisi Makangale katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za SMZ, Mhe:Haji Omar Kheir, akipanda mti mara baada ya kukifungua wa kituo cha Polisi Makangale, ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 KATIBU mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe;Meja Jenerali Projesta Rugasira, akipanda mti mara baada ya ufunguzi wa Kituo cha Polisi Makangale, katika shamra shamra za miaka 53 ya Mpainduzi ya Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe;Omar Khamis Othaman, akizungumza na wananchi wa makangale mara baada ya kuzinduliwa kwa kituo cha Polisi kijijini hapo, ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji, akizungumza na wananchi wa makangale mara baada ya kuzinduliwa kwa kituo cha polisi kijijini hapo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 KAMISHNA wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame, akielezea mikakati ya Jeshi la Polisi Zanzibar, huko katika kijiji cha Makangale mara baada ya kuzinduliwa kwa kituo cha Polisi, katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
KATIBU mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe;Meja Jenerali Projesta Rugasira, akizungumza na wananchi wa makangale mara baada ya kuzinduliwa kwa kituo cha polisi kijijini hapo, ikiwa ni shamra shamra za miaka ya 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.