Habari za Punde

Mgomo baridi wa Wafanyabiashara soko la Chakechake wagoma kuhamia soko jipya Michakaini

Na Mwandishi wetu

Shughuli mbalimbali za kibiashara katika soko la Qatar, Chake chake kisiwani Pemba jana zimesimama kwa siku nzima kwa kile wafanyabiashara hao wanachokiita  kufanya tahmini ya tabia na mwenendo wa biashara zao na mustakbali wao wa kibiashara wa siku za mbeleni.

 Tukio hilo ambalo linaonekana dhahiri kuwa ni mgomo mbele ya macho ya jamii ambao ni baina yao na ofisi ya baraza la mji chake kupinga kwenda katika eneo tengefu linalodaiwa kutokuwa na miundombinu lililobatizwa jina la soko la kuweit huko Michakaini, waligoma kuliita mgomo.

Wamesema wanachokiangalia ni kuwa wameshafanya biashara kwa muda mrefu na sasa niwakati wa kujitathmini kwani kuna mambo mengi yamekuwa nitatizo kwao likiwemo suala la mikopo ya riba iliyo mikubwa jambo ambalo wamelitaja kuwa ni miongoni mwa mambo yanayowatatiza.

 Aidha wamesema pia wanaipa serikali nafasi ya kujitathmini kwa kuona umuhimu wa wafanyabiashara na kuona namna ya kuwaendeleza badala ya kuwakandamiza.

Msemaji wa wafanyabiashara hao ndugu; Salim Moh'd Rashid Calos  hakusita kusema kuwa chama cha mapinduzi (CCM) kinachoongoza serikali nacho kikae na kujitathmini kwani katika ilani yake amesema kuwa suala la kuwapatia wanachi ajira ni miongoni mwa vipaumbele vyake hivyo waone jinsi wafanyabiashara na wananchi wanaojiajiri wenyewe wanavyohangaika na kuona umuhimu wao na nafasi yao katika jamii.

Akifafanuwa alipoulizwa juu ya wafanyabiashara hao kwenda kuhamia katika eneo tengefu lililowekwa kwa ajili ya kufanywa soko huko Michakaini amesema kamwe hawatokwenda kuhamia na wapo tayari kubaki majumbani mwao kama ambavyo wamekuwa wakiambiwa na baadhi ya viongozi wa baraza iwapo watakataa kwenda huko.

Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la mji chakechake Nassor  amesema kilichofanyika leo ni mgomo na si chenginecho na kuwataka wafanyabiashara hao kuitikia wito wa baraza na kama wana  malalamiko yeyote wasisite kuyafikisha serikalini akiwataja wahusika wa hayo kuwa ni mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa kwa ngazi ya chini na hata kwa raisi waweze kufika ikiwa hawajaridhika ili kupatiwa ufumbuzi wa tatizo lao.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mvutano baina ya wafanya biashara wa soko la Qatar kupinga amri ya baraza ya kuhama walipo na kuhamia eneo jipya la Michakaini.

Kwa madai yakuwa eneo hilo si salama kwa maisha na mali zao kutokana na kuwa eneo hilo ni bonde na juu yake kuna barabara yenye mpindo mkali ambayo ni juzi tu gari moja ilipindukia katika bonde hilo na aidha wamesema kuwa eneo hilo ni nje ya mji huku wakilalamikia kutokuwapo na miundo mbinu rafiki ya kuwawezesha kufanya shunghuli zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.