Habari za Punde

Watendaji Serikalini watakiwa kubadilika





Na Salmin Juma, Pemba


Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Salama Mbarouk Khatibu amewataka watendaji wa Serikali kubadilike katika utendaji wao wa kazi ili waweza  kufanya kazi  kwa ufanisi zaidi na kila mmoja atekeleze majukumu yake ipasavyo  ya kazi na  kuacha  tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.

Kauli hiyo ameitowa wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wa serekali mara  baada ya kumaliza kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kusherehekea miaka 53 ya mapindunzi  ya Zanzibar huko katika uwanja wa tensi chake chake.

Amesema kuwa lengo la kufanya usafi ni kuweka mazingira bora  katika Maofisini hivyo ni vyema  wafanyakazi wanapohitajika kuonesha  ushirikiano wao katika kutekeleza majukumu hayo.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka watendaji wa Serekali kuelewa kwamba mapindunzi ya mwaka 1964 ndio yaliyofanikisha  uwepo wa wananchi kutokana na hekma za wazee waliokwisha tangulia hivyo ni vyema kuyathamini  na kuyaenzi matunda hayo ya Mapinduzi  na kuendelea kudumisha   amani na utulivu ndani ya nchi  .

Kwa upande wake Afisa Mdhamini ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais,  Ali Salum Matta amesema kuwa sherehe za Mapindunzi zinalenga zaidi uzinduzi  wa  miradi mbali mbali ya maendeleo hivyo Serekali imejipanga kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo kwa nia ya  kuwaletea maendeleo  wananchi wake .

Aidha amewataka watendaji wa Serekali kushiriki kikamilifu katika sherehe hizo za uzinduzi wa miradi mbalimbali ya kijamii ambayo itanzia rasmi tarehe 02  kwa wilaya zote za Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.