Habari za Punde

Balozi wa India Nchini Tanzania Aahidi Kusaidia Sekta ya Elimu Tanzania

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akiteta jambo na Meneja wa Kampuni ya uwakala wa vyuo vya nje, Global Education Link tawi la Dodoma, Hemed Mlapakolo (mwenye shati jeupe). Kushoto ni Balozi wa India  Sandeep Arya
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.Mizengo Pinda akizungumza jambo wakati alipokuwa akitembelea maonesho hayo akizungumza na Meneja wa Kampuni ya Uwakala wa Vyuo vya Nje, Global Education Link Tawi la Dodoma, Hemed Mlapakolo akiwa na Bolozi wa India Nchini Tanzania Balozi Sandeep Arya, maonesho hayo yanafanyika Mkoani Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akisaidia kitabu cha wageni alipotembelea banda ya maonyesho ya Kampuni ya Uwakala wa vyuo vya nje ya Global Education Link juzi. Kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Meneja wa GEL Dodoma, Hemed Mlapakolo akizungumza jambo kwenye maonyesho ya biashara


Na Mwandishi wetu, Dodoma
KUTOKANA na Tanzania kujikita kufufua uchumi katika sekta ya viwanda vya kati, Balozi wa India nchini, Sandeep Arya, ameihakikishia Tanzania kuisapoti kwenye suala la elimu kwa lengo la kuinua uchumi.
Akizungumza wakati akizindua maonyesho ya biashara yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Kilimo na Wenye Viwanda (TCCIA) mkoani Dodoma kwa kushirikiana na kampuni ya Global Education Link ya Tanzania juzi (jana), Balozi Arya alisema kukua kwa kasi uchumi wa India, kulitokana na kuwapo vyuo vingi vya elimu vyenye vifaa vizuri vya kufunduishia nchini humo.
“Kiwango cha elimu kinachotolewa India ni cha hali ya juu kutokana na upatikanaji wa vifaa vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia, jambo linalowahakikishia wahitimu kutoka vyuo mbalimbali kupata kazi kwa urahisi,” alisema Arya na kuwashauri wanaotaka kusoma nje kuwasiliana na Global Education Link kwa vile wana ushirikiano wa karibu na ubalozi huo.
Alisema suala la utandawazi na mahusiano baina ya nchi hiyo na nyingine katika kurahisisha upatikanaji wa mahitaji muhimu, linachangia kuwakutanisha watu wa aina mbalimbali kupata elimu kutokana na kuwapo na vifaa vilivyopo.
Balozi Arya aliwahakikishia washiriki wa maonyesho hayo kuwa upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya kufundishia nchini India, kumesaidia kutolewa kwa kiwango cha juu cha elimu.
Aidha, alisema baadhi ya mashirika makubwa duniani, viongozi wake walifanikiwa kusoma nchini India na kupata elimu iliyo bora.
Ubalozi wa India umeanzisha ushirikiano na GEL katika kuwasaidia Watanzania wanaotaka kusoma nje ya nchi hasa baada ya ubalozi huo kujiridhisha na namna kampuni hiyo ya uwakala wa vyuo vya nje inavyowafuatilia wanafunzi wake hata baada ya kuwaunganisha na vyuo vya nje kujua maendeleo yao.
Naye Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda aliyekuwa mgeni rasmi katika tukio hilo aliwataka watanzania kujiimarisha katika ujuzi akisema ndio msingi wa kila kitu.
Baadhi ya wanufaika wa elimu kupitia Kampuni ya Uwakala wa vyuo vya nje, Global Education Link (GEL), akiwamo Pelagia Mauma, alisema alifanikiwa kupata elimu bora nchini India kupitia kampuni hiyo kwa gharama iliyo nafuu zaidi.
“Gharama za elimu katika vyuo vyua India ni nafuu zaidi, hawa wenzetu hawaangalii ada bali wanachoangalia ni vipi mtu atafanikisha kupata elimu iliyo bora,” alisema Mauma.
Afisa Mtendaji wa TCCIA mkoa wa Dodoma, Fred Azaria pamoja na kueleza shughuli za chama chake, alisema wanalenga kupunguza umaskini kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma baada ya kuandaa maonyesho ya vifaa vya shule na zana za kufundishia kutoka India.
“Nawaomba Watanzania waweze kutumia fursa iliyopo ya kupata elimu, huku wakiwaomba Watanzania kutumia fursa hiyo kujipatia elimu nchini India,” alisema. 
Nae Meneja wa GEL tawi la Dodoma, Hemed Mlapakolo alisema sababu ya kushirikik maonyesho hayo ni kutoa nafasi kwa Watanzania kuhusiana na namna gani mtu anaweza kufanya uchaguzi sahihi wa kozi ya pale anapotaka kusoma nje ya nchi.
“Tumekuwa mawakala wa vyuo vya nje kwa zaidi ya miaka kumi sasa, wengi wamekuwa wakipitia kwetu kuunganishwa na vyuo vya nje, tumeona tuje hapa ili waweze kupata ufahamu zaidi kuhusiana na uchaguzi wa vyuo vya nje na uchaguzi wa masomo ya kusomea pia,” alisema Hemed.
Hemed alifafanua kuwa kumekuwa na changamoto kubwa kwa Watanzania katika uchaguzi wa nini cha kusoma. “Utakuta wengi wanachojua ni udaktari, lakini kwenye udaktari kuna wa aina nyingi, kuna udaktari wa magonjwa ufahamu, udaktari wa meno tu, udaktari wa mifupa na kadhalika, kazi yetu ni kutoa ushauri wa aina hii. Tunafanya hivi ili kukumbushana kwa sababu kama wengi watakuwa kwenye fani au utaalamu wa aina moja, maana yake ni kwamba fani nyingine zitakosa wataalam au zitakuwa na wataalam wachache,” alisema.

IMETOLEWA NA IDARA YA MAWASILIANO
GLOBAL EDUCATION LINK
DAR ES SALAAM
LEO TAREHE 5 FEB 2017
SIMU: 0712183282
www.gel.co.tz



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.