Habari za Punde

Benki ya NMB Yaipiga Tafu Wizara ya Elimu Zanzibar Kwa Kukabidhi Msaada wa Computer 50 Kwa Ajili ya Skuli za Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Tanzania Bi Ineke Bussemaker akimkabidhi msaada wa Computer 50 Waziri wa Elimi na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma kwa ajili ya Matumizi ya Skuli za Zanzibar hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika majengo ya Wizara ya Elimu Mazizini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akiangalia moja ya Computer 50 zilizotolewa na Benki ya NMB Tanzania kwa matumizi ya Skuli za Zanzibar, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NMB Tanzania Bi Ineke  Bussemaker, wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano ya Computer hizo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Bi Ineke Bussemaker na kulia Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam Bi Vicky Peter Bishudo, wakizungumza wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu mazizini Zanzibar. 
Mkurugenzi Mkuu Benki ya NMB Tanzania Bi Ineke akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa Computer 50 kwa ajili ya Skuli za Zanzibar zilizotolewa na Benki ya NMB Tanzania. hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Tanzania Bi Ineke Bussemaker akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi msaada wa Computer 50 kwa Wizara ya Elimu Zanzibar kwa matumizi ya Skuli mbalimbali za Unguja na Pemba.
Baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Elimu Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo.






No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.