Habari za Punde

CUF yamvua uanachama mwanachama mkongwe katika mkutano wa dharura

Na mwandishi wetu

Chama cha wananchi CUF leo hii kimemfukuza uanachama mwanachama wake mkongwe aliyewahi kushika nafasi mbali mbali za uongozi ndani ya chama hicho, zikiwamo za ubunge na uwakilishi nd; Mussa haji Kombo.

Tukio hilo limetokea mapema jioni ya jana  huko katika tawi la Miembeni, lilolopo mtoni chake chake Pemba kupitia mkutano mkuu wa dharura ulioitishwa.

Mwenyekiti wa tawi hilo bwana Hakimu Mbarikiwa amethibitisha kufukuzwa uwanachama bw; Kombo akisema usaliti  pamoja na kukiuka misingi ya chama pamoja na   kukikashifu chama na katibu mkuu wake  M aalim Seif  Sharifu Hamad kupitia vyombo vya habari kimewasukuma kumuondosha kabisa katika chama hicho.

Amesema mpaka kufikia jana Kombo alikua ni mwanachama wa kawaida ambaye hakuhitaji kufukuzwa uwanachama kupitia vitengo vyengine vya ndani ya chama hicho zaidi ya tawini alikochukulia uanachama, hivyo tawi lake kupitia wanachama wameliona hilo na kuchukuwa hatua rasmi ya kumfukuza uanachama leo hii.

Nae Mwenyekiti wa jimbo la chake chake maalim Shaaban Mussa amesema  wamelipokea suala hilo kwa mikono miwili na kulipa baraka zote, huku akidai kuwa Mussa Haji kwa sasa hakuwa mwenye kustahili kubaki ndani ya chama hicho kwa usaliti aliofanya na kuwataka wananchi na wanachama wa CUF kutambua na kupokea tarifa za kufukuzwa kwake.

Jumla ya wanachama 56 kati ya 100 walio naithibati ya kumfukuza uwanachama mwanachama yeyote ndani ya chama kupitia tawi la miembeni walipiga kura za kumkataa na kumfukuza uanachama bw; kombo jana.

Akizungumza katibu wa jimbo la chake chake bw; Juma Mohammed Mwachawa amesema kifungu cha 2 (1) ambacho kinazungumzia masharti ya mwanachama kupitia katiba  ya chama hicho kimewaruhusu wanachama kumfukuza uanachama bw; Kombo kwa kukiuka masharti na katiba ya chama hicho.

Bw; Mussa Haji Kombo aliwahi kushika nyazifa mbali mbali kupitia chama hicho ikiwemo mkurugenzi wa mipango na uchaguzi na mjumbe wa baraza kuu taifa na aidha nafasi mbali za ubunge na uwakilishi kupitia jimbo la chake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.