Habari za Punde

JKU watakiwa kuwajenga vijana kikakamavu na kimaadili

 Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi mhe  Ayoub Mahmoud Mohammed alipokuwa akizungumza na makamanda  wa Jeshi la kujenga uchumi Zanzibar walipoadhimisha kutimia miaka 40 tangu kuanzishwa kwake huko  Makao Makuu ya JKU Saateni 
 Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi mhe  Ayoub Mahmoud Mohammed alipokuwa akiongoza maandamano ya Jeshi la kujenga uchumi Zanzibar walipoadhimisha kutimia miaka 40 tangu kuanzishwa kwake huko  Makao Makuu ya JKU Saateni 

Jeshi la kujenga uchumi Zanzibar JKU limetakiwa kuwajengea vijana ukakamavu,nidhamu na maadili pamoja na stadi za maisha ili waweze kujitegemea na kuifanya jamii kuwa karibu na jeshi hilo.


Akizungumza mara baada ya kumaliza matembezi kuelekea kilele cha maadhimisho ya sherehe za jeshi hilo kutimia miaka 40 tangu kuanzishwa kwake Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mahmoud Mohammed anasema kuwa kabla ya kuasisiwa kwake JKU kulikuwa na utarataibu wa kambi za vijana wa kujitoalea katika shughuli mbali mbali za ujenzi wa taifa.



Mhe.Ayoub amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imo katika mapango wa kurejesha utaratibu wa vijana wanapomaliza masomo ya lazima kupita katika kambi za Jeshi la Kujenga Uchumi kabla ya kuanza shuguli nyengine za kujiendeleza na maisha.

Aidha amelipongeza Jeshi la hilo kwa kuwa wazalendo na kutekeleza maagizo ya Serikali katika shughuli mbali mbali za kijamii na kuwataka kuendelea kusimamia na kudumisha amani na utulivu iliyopo sambamba na kuwashughulikia wale wote wanaoashiria kuvuruga amani ya nchi bila ya kujali wadhifa wao.
Akimkaribisha mgeni rasmi katika sherehe hizo kaimu kamanda Mkuu wa Jku Zanzibar Kanal Ali Hamad Mtumweni amesema Jeshi hilo litaendelea kuwa wabunifu na kusimamia vyema mipango na mikakati waliyojiwekea ili kuhakikisha kikosi kinazidi kuwa imara kwa maslahi ya vijana na taifa kwa ujumla.

Jeshi la kujenga uchumi Zanzibar JKU limetimiza miaka 40 kutoka mwaka 1977 lilipoanzishwa kama kambi ya kuwajenga vijana kimaadili na nidhamu ambapo kilele cha sherehe hizo kinafikia tarehe 3 mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.