Habari za Punde

Kikosi cha Timu ya Zimamoto Yawasili Salama Nchini Msumbiji Kwa Ajili ya Mchezo wao wa Marudiano Utakaofanyika Jumamisi Wiki Hii.

Kikosi cha Timu ya Zimamoto kinachowakilisha Zanzibar katika michuano ya Mabingwa Barani Afrika imewasili salama na kuaza kwa mazoezi ya kuzowea hali ya hali ya Nchi hiyo kwa kujiandaa na mchezo wao wa marudio.

Mchezo wao huo wa marudio na Timu ya Ferroviario unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii siku ya jumamosi utafanyika katika uwanja wa mji wa Beira Msumbiji.

 

Katika mchezo wao wa awali uliofanyika jumamosi iliyopita Zanzibar katika uwanja wa Amaan Timu ya Zimamoto imeshinda mchezo huo kwa mabao 2-1.  

Miongoni mwa mapungufu yaliyoonekana kwa Zimamoto kwenye mchezo huo ni staili ya mabeki wake wakati wa kukaba.


ilionekana fika kuwa ukabaji wa walinzi hao hutoa mwanya kwa mpinzani kwa vile hukaba takriban wachezaji watatu jambao ambalo huenda likawaathiri kama hawatolifanyia kazi.



Zimamoto inahitaji kupata ushindi kwenye mchezo huo wa marejeano au sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.