Mtoto wa Marehemu Abdallah Khelef Shauri (DULLA) Sofia Abdallah Khelef Shauri akiweka shada la maua la uchungu katika kaburi la Baba yake baada ya kuzikwa leo kwa taratibu zote za Dini ya Kiislam kupitia kwa Jumuiya ya Waislam Watanzania wanaoishi Nchini Norway katika makaburi ya kiislam Skonger.
Familia ya Shauri Mjaka na Ndugu Zake inatowa Shukrani kwa Wananchi Wote walioshiriki kwa njia moja kuungana na familia hiyo katika kipindi chote cha Msiba wa Mtoto wao Abdallah Khefel Shauri (DULLA) katika kipindi kigumu cha msima huo uliotokea Nchini Norway siku ya jumamosi iliopita na kufikia tamati ya kukamilisha shughuli za mazishi zilizofanyika leo Nchini Norway katika majira ya mchana saa 6:00 kwa kuuhifadhi mwili wa marehemu kwa kukamilisha taratibu zote za mazishi katika makaburi ya kiislam Skonger.
Tunatoa shukrani kwa Mzazi mwenziwe Mama Sofia kwa mchango Mkubwa aliotoa kufanikisha maziko hayo. Tunatoa shukrani za dhati kwa Mama Sofia Inshaallah Mwenyenzi Mungu atakujalia kila la kheri katika maisha yako.
Pia na Marafiki waliofika kutoka Nchi jirani na kuwahi msiba huo kumshindikia mpendwa rafiki yao.
Inatowa Shukrani kwa Jumuiya zote za Watanzania weanaoishi Nje kwa umoja wao kwa hali na Mali kuweza kufanikisha suala hii kwa ushirikiano wao. Tunatoa shukrani kwa Uongozi wa Jumuiya watanzania Wanaoishi Nchini Norway kusimamia suala hili hadi mwisho kufanya taratibu za mazishi ya Ndugu yetu Tunatoa Shukrani kwa Jumuiya ya Kiislamu ya Watanzania Norway na Ndugu Hassan,na Jamal kusimamia hadi kukamilika.
Hatuna cha kuwalipa kwa hili inshalla Mwenyenzi Mungu atawajalia kila la kheri na moyo wa imana kwa hili na lengine.
Ameen.
Mtoto wa Marehemu Abdallah Khelef Shauri (DULLA) Sofia Abdallah Khelef Shauri akiweka shada la maua la uchungu katika kaburi la Baba yake baada ya kuzikwa leo kwa taratibu zote za Dini ya Kiislam kupitia kwa Jumuiya ya Waislam Watanzania wanaoishi Nchini Norway katika makaburi ya kiislam Skonger
Mama wa Mtoto Sofia Abdallah Khelef Shauri akiweka shada la maua katika kaburi la mzazi mwezake.
Marafiki na Jamaa wa Watanzania wanaoishi Nchini Norway wakishiriki katika mazishi ya marehe Abdallah Khelef Shauri Mjaka (DULLA) wakiwa katika viwanja vya makaburi ya waislam Nchini Norway leo wakati wa mazishi hayo yaliofanyika alasiri.
Tunamuomba mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amin.
ReplyDelete