1
Wachezaji wa Timu yac KVZ wakishangilia ushindi wao wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar baada ya kuifunga Timu kutoka ya Le Massenger ya Burundi.
Katima mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar na kuhudhuriwa na mashabiki wengi uliofanyika jioni. Timu ya le Massenger imeandika bao lake la kwanza kwa njia ya penelti katika dakika ya 13 ya mchezo huo kipindi cha kwanza baada ya beki wa timu ya KVZ kuushika mpia akiwa katika eneo la golini kwao.
Penelti hiyo hiyo imepigwa na mchezaji Sabu Makoma na kuiandikia bao la kwanza timu yake.
Mchezo ulikuwa wa kila pande kumshambulia mwezake, katika dakika ya 39 ya mchezo huo kipindi cha kwanza timu ya KVZ imepata goli lake la kusawazisha kwa njia ya penenti iliopigwa na mchezaji wake Suleiman Abdi na kuiandikia bao la kusawazisha mchezo uliendelea kwa mashambulizi katika goli la timu ya Burundi na kuwafanya mabeki wa timu ya Le Massengers kupata kazi ya ziada kuokoa mochumo ya washambuliaji wa Timu ya KVZ, katika dakika ya 42 ya mchezo huo kipindi cha kwanza timu ya KVZ imeandika bao lake la pili kupitia mshambuliaje wake Sultani Juma kwa kuunganisha krosi.
Hadi mwisho wa mchezo huo timu ya KVZ imetoka kifua mbele kwa ushindi wa bao 2-1.
Kikosi cha Timu ya KVZ kilichoiendesha mchaka mchaka Timu ya Le Massenger ya Burundi katika mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu ya KVZ imeshinda mchezo huo kwa mabao 2-1.
Kikosi cha Timu ya Le Massenger ya Burundi kilichokubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Timu ya KVZ ya Zanzibar katika mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kocha wa Timu ya Le Massenger ya Burudi akiwa na simanzi baada ya timu yake kukubali kipigo cha mabao 2-1 na Timu ya KVZ ya Zanzibar katika mchezo wa hatua ya mwanzo ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika mchezo uliofanyika Uwamja wa Amaan Zanzibar.
No comments:
Post a Comment