Habari za Punde

Wananchi wa Kijiji cha Kendwa Shehia ya Kiwani Wakijenga Tuta kwa Ajili ya Kuzuiya Maji ya Chumvi Kuingia Katika Mashamba Yao.

 Wananchi wa Kendwa Shehia ya Kiwani Kisiwani Pemba, wakiwa katika harakati za kupiga Tuta la kuzuwia Maji ya Chumvi yasiingie katika mashamba yao ya Kilimo cha Mpunga ambapo Mwaka uliopita Wakulima hao walikosa Mavuno kwa Kilimo hicho kuvamiwa na maji ya Chumvi na mkondo mkubwa wa maji ya Mvua ambapo jumla ya Wakulima zaidi  ya 270 watanufaika na Tuta hilo kwa kurejea mashambani.
Wananchi wa kijiji cha Kendwa Shehia ya Kiwani Pemba, wakiwa katika harakati za kujenga Tuta ili kuzuiya maji ya chuvi kuingia katika mashamba yao. Kutokana na kuingia kwa maji ya chuvi wakulima wa bonde hilo mwaka jana wameshindwa kulima mpunga kwa mashamba yao kuvamiwa na maji ya chumvi
Tuta la kuzuwia maji ya Mvua katika Shehia ya Kiwani Pemba, likiwa limefikia hatuwa ya kuridhisha ambalo litookowa ekari 98.1 ya mashamba ya kilimo cha Mpunga ambayo huvamiwa na maji ya Chumvi na Wakulima kukosa mazao.

Baadhi ya Mashamba ya Wakulima wa Kendwa Kiwani Pemba , ambayo huathiriwa na maji ya Chumvi na kuwakosesha Wakulima kukosa mavuno ya Mpunga .

Picha na Bakar Mussa-Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.