Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Awasili Zanzibar Akitokea Nchini India Akiwa Katika Ziara ya Kiserekali.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake ya Wiki Mopja Nchini India.
Kulia ya Mh. Ayoub ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwemyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Issa Haji Gavu na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Dr. Sira Ubwa Mamboya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Issa Haji  Ussi Gavu akimkaribisha Balozi Seif mara tu baada ya kuwasili Zanzibar.
Wa kwanza kutoka Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Rashid Ali Juma.
Mjumbe wa Baraza na Mapinduzi ambae pia ni Waziri asiye na Wizara Maalum Mh. Said Soud akimlaki Balozi Seif katika mapokezi hayo.
Kulia ya Mh. Soud ni Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiye na Wizara Maalum Mh. Ali Juma Khatib na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib.
Balozi Seif na Mkewe wakimalizia kusalimiana na Viongozi mbali mbali wa serikali waliofika kuwapokea wakitokea Nchini India.(Picha na – OMPR – ZNZ.)
Na Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewasili Zanzibar mapema leo asubuhi akitokea nchini India ambako alifanya ziara ya wiki moja.
Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Balozi Seif aliyeambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi alipokewa na Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Watendaji wakuu wa Serikali pamoja na baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa.
Balozi Seif ambae aliuongoza Ujumbe wa Mawaziri wawili, Naibu Waziri  na Makatibu wakuu alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi na Makampuni mbali mbali ya vitega uchumi.
Miongoni mwa Taasisi na makampuni hayo ni yale yanayojishughulisha na sekta ya Afya,Kilimo pamoja na Makampuni ya ujenzi.
Ziara ya Balozi Seif na Ujumbe wake imeonyesha matumaini makubwa kutokana na Taasisi na baadhi ya Makampuni kuonyesha nia na muelekeo wa kutaka kuzitumia fursa za uwekezaji zilizopo Visiwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.