Habari za Punde

Mchezo wa Ufunguzi wa Kombe la Karume Cup Uwanja wa Gymkhana Kasti ya Timu ya Mafunzo na African Magic Wanawake Mpira wa Kikapu. Timu ya Mafunzo Imeshinda kwa Vikapu 56-49.

Mchezaji wa Timu ya Mafunzo akimpita mchezaji wa Timu ya African Magic, wakati wa mchezo wao wa kwanza wa Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Karume Cup Wanawake mchezo uliofanyika katika uwanja wa Gymkhana Zanzibar Timu ya Mafunzo imeshinda kwa Vikapu 56 - 49.

Katika mchezo huo wa ufunguzi uliofanyika leo jioni timu hizo zimeonesha mchezo wa hali ya juu kwa mchezo safi na wa kujiamini kila upande kwa kuonesha umahili wa kujiandaa na michuano hiyo ya Karume Cup.kwa upande wa Wanawake.

Kipindi cha robo ya kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa na vikapu 15 - 14 Timu ya Mafunzo ilikuwa ikiongoza kwa kikapu kimoja   

Katika robo ya tatu timu hizo zilikuwa na Vikapu 25 - 27 Timu ya Mafunzo ilikuwa mbele hadi kipenga cha mwisho wa mchezohuo timu ya mafunzo imetoka kifua mbele kwa vikapu 56 - 49.

 Michuano hiyo itaendelea kesho kwa michezo saa 8 kati ya New West Vs KVZ  na saa 10 kutakuwa na mchezo kati ya Timu za Nyuki na African Magin zote kwa upande wa Wanaume.

Timu zinazoshiriki kwa Upande wa Wanawake ni Duma, Mafunzo,JKU,KVZ na African Magic.

Kwa upande wa Timu za Wanaume Kundi A litakuwa na Timu Beit El Ras, KVZ, Rangers, Polisi Mbuyuni na New -West 

Kwa upande wa Kundi B litakuwa na Timu za Nyuki, Usolo, African Magic, JKU, Stone Town na Zanzibar Kwerekwe.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.