STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 26.03.2017
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein
ameutaka uongozi wa Taasisi ya “Zanzibarlicious Women Group” kuongeza kasi ya
kuendeleza shughuli zao kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
na Taasisi nyengine katika kupambana na vitendo vya udhalilishaji wanawake na
watoto.
Mama Shein aliyasema
hayo katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla ya muendelezo wa Siku ya
Wanawake duniani, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hilton Double
Tree, Shangani mjini Zanzibar.
Katika hotuba yake hiyo,
Mama Shein alisema kuwa ni dhahiri kwamba jitihada za kuwasaidia wanawake
wapate uwezo zaidi wa kufanya shughuli zaidi za kujiongezea kipato haziwezi
kufanikiwa iwapo wataishi na hofu ya kufanyiwa vitendo udhalilishaji wao aau
watoto wao.
Hivyo Mama Shein alisema
kuwa taasisi hiyo ni vyema ikawa na mikakati madhubuti na kuungana na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar katikakupambana na vita hivyo.
Kwa kujua changamoto
zinazowakabili watoto katika maisha yao Mama Shein alaisema kuwa jitihada za
makusudi zinahitajika ili wasipoteze matarajio waliyonayo na kuwataka wazazi waendelee
kuwaongoza, kuwafunza maadili mema kwa mujibu wa mafunzo ya dini silka na
utamaduni wa Kizanzibari huku akiwataka watoto kuongeza bidii katika masomo
yao.
Aliongeza kuwa jambo la
kutia moyo ni kuwa Taasisi hii pia, inashughulikia ustawi wa watoto na hasa
watoto wa kike na kueleza furaha yake kwa Taasisi hiyo imelitambua jukumunhilo
wakiwa wanawake kwa kuwashughulikia waoto wao katika masuala mbali mbali
yanayohusu ustawi wao.
Mama Shein alitoa wito
kwa Taasisi hiyo kutokata tama kutokana na kukabiliwa na changamoto mbali mbali
katika majukumu yao na kuwataka kuzitumia changamoto hizo kuwa ni fursa za
kuwaletea maendeleo.
Alisekama kuwa jitihada
za taasisi hiyo zinakwenda sambamba na mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein katika kuwawezesha
wanawake waliojiajiri wenyewe kwa lengo la kujiongeze kipato.
Sambamba na hayo, Mama
Shein alitoa pongezi kwa Taasisi hiyo kwa kazi nzuri ambayo imekuwa ikiifanya
tangu ilipoanzishwa na kuwataka kutambua kwamba Serikali inathamini sana kazi
nzuri inayofanywa na Taasisi hiyo katika jamii.
Risala ya Taasisi hiyo
ya wanawake iliyoanzishwa mwaka 2011 na kusajiliwa rasmi mwaka 2013 ilisomwa na
Mtunza nidhamu wa Taasisi hiyo Shangwe Ramadhan Yussuf,ambayo ilieleza nia yake ikiwa
ni kumuendeleza na kumuwezesha mwanamke kiuchumi, kijamii na ,imwenendo.
Aidha, risala hiyo
ilieleza, changamoto, mafanikio na malengo ya Taasisi hiyo ambapo miongoni mwa
malengo yake ni pamoja na kutoa eleimu ya ujasiriamali kwa vikundi mbalimbali
vya wanawake na kuwawezesha kubuni biashara ndoho ndogo na jinsi ya kuweza
kutafuta mitaji kutoka taasisi mbali mbali za kitaifa.
Mapema Waziri wa Kazi,
Uwezeshajai Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, Moudline Castico alitia pongezi
kwa Taasisi hiyo na kueleza kuwa Wizara yake iko tayari kuendelea kutoa
ushirikiano na Taasisi hiyo na nyenginezo zenye malengo kama hayo.
Pamoja na hayo, Waziri
huiyo alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Dk. Shein kwa kutimiza mwaka mmoja
tokea kuingia madarakani katika awamu ya pili ndani ya Serikali ya Awamu ya
Saba kutokana na ushisndi wa kishindo alioupata katika uchaguzi uliopita.
Nae Mlezi wa Taasisi
hiyo ambaye pia, ni Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kiombo alieleza historuia
fupi ya Taasisi hiyo na kupongeza juhudi inazozifanya katika kufikia malengo yake
na kusisitiza haja ya kuungwa mkono ili izidi kupata mafanikio zaidi.
Katika hafla hiyo
michango ya harambee ilifanyika ambapo Mama Shein akiwa mgeni rasmi alichangia
Tsh. Milioni moja pamoja na kugawa vyeti
maalum kwa watu maalum kwa juhudi zao za kuiunga mkono taasisi hiyo.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment