Habari za Punde

Rais Dk Shein afanya uteuzi wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mamlaka ya Kudhibiti Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar.



Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 17 cha sheria ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia namba 6 ya mwaka 2016, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, amemteua Bwana Omar Zubeir Ismail kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mamlaka ya Kudhibiti Utafutaji na Uchimbaji wa mafuta na gesi asilia, Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo, Bwana Omar Zubeir Ismail alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Idara ya Nishati, Zanzibar.

Uteuzi huo uliosainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, umeanza leo tarehe 18 Machi 2017.


IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO-ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.