Habari za Punde

Wanafunzi watakiwa kuwa makini ili kujiepusha na vitendo vya udhalilishaji

Na Salmin Juma

Kutokana na kukithiri kwa matendo ya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia nchini  yakiwamo ya ulawiti na ubakaji, Jumuiya ya Haki Jamii (HAJA) kisiwani Pemba inayoshuhulika na utowaji wa elimu juu ya matendo hayo maovu imewaasa wanafunzi  kua makini na kujiepusha na kila sababu  inayoweza kuzuilika ya kumfanya kufikwa na matendo hayo ikiwemo kujiingiza katika mapenzi, wakati bado muda haujafika

Akitoa mafunzo ya madhara ya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa skuli ya sekondari Chanjamjawiri msadizi katibu wa Jumuiya hiyo bw: Issa Ali Khamis amesema kua, matendo ya udhalilishaji nchini yanaonekana kushamiri kiasi ambacho imekua ni hatari kwa watoto wakiwamo wanafunzi.

Amesema kua, ni wajibu wa kila mwanafunzi kushuhulikia masomo na kuachana na mapenzi kwani nayo yanaonekana ni moja kati ya sababu zinazopelekea mtoto kuingia katika ya udhalilishaji wa kijinsia.

Katika suala la  liwati linaloonekana kushamiri katika jamii amefahamisha kuwa, kutokana tafiti mbalimbali zilizofanywa na wadau zinaonyesha kuwa liwati ni vitendo vinavyoonekana kutuwama nchini huku akitoa wito kwa jamii kwa kusema kua miongoni mwa wahanga wa matukio hayo ni watoto hivyo ni wakati wa kua mstari wa mbele kutoa ushahidi mahakamani na mashirikiano mengine ili kufanikisha kutokomeza matendo hayo.

Akiwasilisha mada ya athari za Liwati kwa aliyefanya au kufanyiwa mwanachama wa Jumuiya hiyo Nd: Ali Maisara Kombo amesema kua, tatizo kubwa linalompata mtu  ni kuharibika kisaikologia.

Amesema ikitokea mwanafunzi amefanyiwa kitendo hicho kwa kiwango kikubwa hatoweza kufanya vizuri katika masomo yake kwani muda mwingi atautumia kuwaza ukatili huo.

"ukifanyiwa  au ukifanya kitu cha kwanza unaharibika kisaikologia hata kama ulikua unasoma vizuri chemistry na biology basi huwezi kuwaza masomo, kutwa utakumbuka hicho kitendo, pia mwili kama ni mwanaume utaregemea na baadae utapewa majina mengine mabaya " alisema Kombo
Kwa upande wao wanafunzi wameonyesha kufurahika na mafunzo hayo.

Atqa Sultan Salim (kidato cha pili) amesema kua, mafunzo waliyoyapata yamewajenga kua na ari ya masomo na kuachana na kila kisichowahusu kwakua muda bado haujafika.

Suleiman Daud Birol  (kidato cha nne) amesema , kutokana na umuhimu mada zilizojadiliwa haitoshi elimu hiyo kutolewa kwa kipindi kirefu na badala yake jumuiya iandae utaratibu wa kila mwezi kuwapitia na kuwakumbusha juu ya madhara ya udhalilidhaji na ukatili wa kijinsia.

Jumuiya ya Haki Jamii imepanga kuwafikia wanafunzi wa skuli tofauti kisiwani Pemba kuwapa mafunzo juu ya madhara ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia ili wapate kujipesha na vichecheo vinavyoweza kuepukika

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.