Habari za Punde

Mabalozi wa CCM wanaomaliza muda wao jimbo la Kiembesamaki waagwa

 Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Ramadhan Mrisho Rupiya akizungumza na mabalozi wa jimbo hilo kuhusu mabadiliko ya katiba ya chama chao katika mkutano wa kuaga mabalozi waliomaliza muda wao uliofanyika ukumbi wa tawi la ccm Kiembesamaki.

 Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki ambae pia ni Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akiagana na mabalozi waliomaliza muda wao na kuwaomba waombe tena nafasi hiyo.
  Baadhi ya mabalozi wakimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo alipokua akiagana nao.
Katibu wa Jimbo la Kiembesamaki Mzee Mtumwa Abdalla akionyesha fedha zilizotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesaki Mahmoud Thabit Kombo kwa mabalozi wote ambapo kila balozi  alipatiwa shl. 20,000/=.

Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.